Featured Michezo

AL AHLY YACHAPWA NYUMBANI NA MAMELODI SUNDOWNS LIGI YA MABINGWA AFRIKA

Written by mzalendoeditor

MABINGWA watetezi wa Kombe la klabu bingwa Afrika timu ya Al Ahly imeshindwa kutamba katika uwanja wake baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Mamelodi Sundowns mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa wa Cairo nchini Misri.

Shujaa wa Mamelodi Sundowns alikuwa Thapelo Morena dakika ya 86 aliwanyanyua mashabiki wake baada ya kuachia shuti kali na kujaa wavuni na kumuacha mlinda mlango  Mohamed El-Shannawy hana la kufanya.

Kwa ushindi huo Mamelodi wamefikisha Pointi 7 na kuendelea kuongoza msimamo wa kundi A wakiwa wamecheza mechi tatu huku Al Ahly wakibaki nafasi ya tatu wakiwa na Pointi 1 wakicheza mechi mbili,nafasi ya pili inashikiliwa na Al-Merreikh wakiwa na Pointi 4 na Al Hilal Omdurman wanashika mkia wakiwa na Pointi 1.

About the author

mzalendoeditor