Featured Kimataifa

“EXPO2020DUBAI YAIWEKA TANZANIA KATIKA RAMANI YA DUNIA” -WAZIRI  NDUMBARO

Written by mzalendoeditor
 Baadhi ya Wasanii  kutoka Tanzania wakiwa kwenye banda la Tanzania katika Maenesho Makubwa ya Kibiashara  Expo 2020 Dubai wakitumbuiza ili kuwavutia wageni mbalimbali kutembelea Banda hilo katika Maonesho hayo yanayoendelea
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akiwa na  watalii  ambao  wakiangalia Mubashara wanyama katika Eneo la Hifadhi ya NgoroNgoro kupitia App ya NgoroNgoro Live ambapo imekuwa kichocheo kikubwa cha watalii kutembelea Banda la Tanzania
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akifanya mahojiano na Mwandishi wa TBCI, Vumilia Mwasha  huku akiwaelezea watalii ambao walikuwa wakiangalia Mubashara wanyama katika Eneo la Hifadhi ya NgoroNgoro kupitia App ya NgoroNgoro Live ambapo imekuwa kichocheo kikubwa cha watalii kutembelea Banda la Tanzania
Baadhi ya wageni mbalimbali waliofika katika Banda la Tanzania wakiangalia picha za vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania mara baada ya kutembelea katika Banda la Tanzania katika Maonesho Makubwa ya Kibiashara ya Expo2020 Dubai
Kamishna Uhifadhi wa TANAPA, Simoni Mwakilema ( kushoto) akiwa na Kamishna Uhifadhi wa TAWA, Mabula Misungwi wakiangalia picha mbalimbali katika Banda la Tanzania mara baada ya kutembelea Banda la Tanzania  katika Maonesho Makubwa ya Kibiashara ya Expo2020 Dubai
Balozi wa Tanzania wa nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu, Mhe. Mohamed Mtonga    ( wa tano kushoto)  akiwa na Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Dkt. Francis Michael ( katikati) pamoja na Katibu Mkuu wa Sanaa, Utamaduni  na Michezo, Dkt. Hassan Abbas ( wa tano kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja na  Baadhi ya Wasanii kutoka Tanzania wakiwa nje ya Banda la Tanzania
……………………………………………………..
NA MWANDISHI WETU, DUBAI.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro amesema Maonesho ya Kibiashara ya  Expo2020 Dubai yanazidi kuiweka Tanzania katika ramani ya dunia kutokana na Watu wa Mataifa mbalimbali Dunia kujua Hifadhi za Tanzania ikiwemo Hifadhi ya Serengeti, NgoroNgoro, Madini ya Tanzanite, Mlima Kilimanjaro yapo Tanzania na sio nchi jirani.
Hatua hiyo inakuja kufuatia upotoshwaji wa muda mrefu  ambao umekuwa ukifanya na baadhi ya nchi za jirani kuwa kila vivutio vizuri vya utalii ambavyo vipo Tanzania huwahadaa watalii kuwa vipo nchini mwao.
Akizungumza mapema leo, Dkt. Ndumbaro amesema watu mbalimbali ambao wamekuwa wakitembelea Banda la Tanzania wamekuwa wakishangaa kuona madini ya Tanzanite, Hifadhi ya Serengeti, Mlima Kilimanjar pamoja na Hifadhi ya NgoroNgoro kuwa zipo Tanzania.
” Nimekuwa nikizungumza  na wageni mbalimbali wanaotembelea Banda ka Tanzania wengi wao wamekuwa wakishangaa na   kukiri kuwa mwanzo walikuwa wanajua kuwa vivutio hivyo havipo Tanzania bali vipo nchi jirani”  alisema Dkt. Ndumbaro
“Maonesho haya ya Dubai yameipaisha Tanzania kuwa ni nchi yenye utajiri mkubwa wa vivutio vya utalii ambavyo ni vizuri  tofauti na wenzetu wanaopotosha kuwa ni vyao” alisisitiza Dkt. Ndumbaro.
Miongoni mwa taasisi za Tanzania za Wizara ya Maliasili na Utalii  zinazoshiriki maonesho hayo ni pamoja na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyanapori Tanzania (TAWA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na Wakala wa Huduma za Misitu Tazania (TFS).
Maonesho hayo ya kimataifa yaliyoanza  Oktoba Mosi mwaka 2021 yanaendelea hadi Machi 31 mwaka huu na yameshirikisha zaidi ya nchi 192.

About the author

mzalendoeditor