Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Lawrence Mafuru akihutubia wakati wa uzinduzi wa Timu ya Kitaifa ya Kuwezesha Ugharamiaji wa Miradi ya Maendeleo kwa kutumia njia mbadala (Alternative Project Financing – APF National Facilitation Team) uliofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Lawrence Mafuru akipokea kwa niaba ya Serikali Hundi Kifani ya shilingi milioni 460.4 kutoka kwa Mwakilishi Mkazi wa Mfuko wa Maendeleo ya Mitaji wa Umoja wa Mataifa (UNCDF) Bw. Peter Malika, zitakazoiwezesha Timu ya Kitaifa iliyoundwa kwa ajili ya Kuwezesha Ugharamiaji wa Miradi ya Maendeleo kwa kutumia njia mbadala (Alternative Project Financing – APF National Facilitation Team) kutekeleza majukumu yake kikamilifu.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Lawrence Mafuru akimkabidhi vitendea kazi Kamishna Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Dionesia Mjema kwa niaba ya Timu ya Kitaifa iliyoundwa kwa ajili ya Kuwezesha Ugharamiaji wa Miradi ya Maendeleo kwa kutumia njia mbadala (Alternative Project Financing – APF National Facilitation Team). Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar Bw. Aboud Hassan Mwinyi, kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dkt. Sixbert Mkama pamoja na Kamishina wa Idara ya Maendeleo ya Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Charles Mwamaja, Jijini Dodoma

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Lawrence Mafuru (katikati) akipiga makofi kufurahia jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Timu ya Kitaifa iliyoundwa kwa ajili ya Kuwezesha Ugharamiaji wa Miradi ya Maendeleo kwa kutumia njia mbadala (Alternative Project Financing – APF National Facilitation Team). kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar Bw. Aboud Hassan Mwinyi na kushoto kwake ni Kamishna wa Idara ya Maendeleo ya Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Charles Mwamaja, Jijini Dodoma

Baadhi ya wajumbe wa Timu ya Kitaifa ya Kuwezesha Ugharamiaji wa Miradi ya Maendeleo kwa kutumia njia mbadala wakionesha vitendea kazi walivyokabidhiwa baada ya kuzinduliwa kwa timu hiyo katika tukio lililofanyika Wizara ya Fedha na Mipango katika ukumbi wa Kambarage, Jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Lawrence Mafuru (aliyekaa katikati) kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar Bw. Aboud Hassan Mwinyi na kushoto kwake ni Kamishna wa Idara ya Maendeleo ya Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Charles Mwamaja, wakiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Kitaifa ya Kuwezesha Ugharamiaji wa Miradi ya Maendeleo kwa kutumia njia mbadala (Alternative Project Financing – APF National Facilitation Team), baada ya kuzinduliwa kwa Timu hiyo katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, Jijini Dodoma.

……………………………………………….

Na Alex Sonna-DODOMA

SERIKALI imezindua  timu ya kitaifa ya kuwezesha ugharamiaji wa miradi ya maendeleo kwa kutumia njia mbadala(APF) ili kuwezesha miradi mingi kutekelezeka na kukamilika badala ya kutegemea njia zilizozoeleka katika utekelezaji wa miradi hiyo.

Akizindua timu hiyo leo Februari 24,2022 jijini Dodoma yenye wajumbe 31,Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Lawrence Mafuru, amesema kuwa katika Mpango wa Maendeleo wa taifa wa miaka mitatu serikali imepanga kupata Sh.Trilioni 40.6 kutoka sekta binafsi na jukumu la kufanikisha hilo lipo kwa timu hiyo.

“Serikali imekuwa ikitekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo kwa lengo la kukuza uchumi na kuondoa umasikini kupitia mipango hiyo, miradi mbalimbali ya maendeleo imekuwa ikitekelezwa kupitia Bajeti ya Serikali.

Amesema kuwa mahitaji ya ugharamiaji miradi ya serikali yamekuwa makubwa huku mapato yanayotokana na vyanzo vyake yakikua taratibu kuliko ambavyo mahitaji yanaongezeka.

“Ugharamiaji wa miradi kwa utaratibu huu umekuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ufinyu wa bajeti ya Serikali na hivyo miradi mingi kupata fedha kidogo na kutokamilika kwa wakati. “amesema Mafuru

Mafuru amesema kuwa utekelezaji wa mradi huo ni  utakelezaji wa Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha wa Mwaka 2020/21-2029/30 ambapo miongoni mwa malengo ya Mpango huo ni kuhakikisha upatikanaji wa fedha za muda mrefu kwa ajili ya kugharamia miradi ya kimkakati.

“AFP ni utaratibu wa kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kutumia njia mbadala nje ya utaratibu wa kawaida wa kutumia bajeti ya Serikali. “amesema

Aidha amesema kuwa timu hiyo itakuwa na jukumu la kujenga uwezo wa Wizara, Idara, Taasisi, Wakala, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kuandaa maandiko ya miradi na kufanya upembuzi yakinifu na kuratibu uandaaji wa maandiko ya miradi yatakayogharamiwa kwa njia mbadala na kuratibu utoaji wa elimu kwa umma.

“Mambo ya kuandaa maandiko tutumie wataalamu waliopo ikiwamo mabenki yana timu za wataalamu ambao watasaidia miradi yetu, natoa wito kwa wadau wote wa fedha kuendelea kutoa ufadhili wa utekelezaji wa miradi ya serikali,”amesisitiza

Aidha amesema utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (FYDP III) utagharimu kiasi cha Shilingi trilioni 114.9 ikijumuisha Shilingi trilioni 74.3 kutoka sekta ya umma na shilingi trilioni 40.6 kutoka sekta binafsi.

“Hivyo, ni wazi kuwa utaratibu huu ni muhimu sana katika kipindi hiki ambacho Serikali inatekeleza miradi mikubwa ya kimkakati.”amesema

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Switbert Mkama, amesema kumekuwapo na miradi mingi nchini lakini ina kikwazo cha maandiko hivyo kupitia timu hiyo anaamini itaibua miradi inayoweza kukopesheka kwa halmashauri.

Naye Mwakilishi Mkazi wa shirika la  Maendeleo la Mitaji la Umoja wa Mataifa Umoja wa Mataifa (UNCDF) Bw. Peter Malika, amesema,shirika hilo limetoa ruzuku ya shilingi milioni 460 ili kuiwezesha  Timu hiyo ya Kitaifa kuandaa miradi kupitia vyanzo mbadala vya fedha.

Previous articleWIZARA YA AFYA YAKABIDHI MASHINE ZA KUCHANGANYA CHUMVI NA MADINI JOTO TAMISEMI.
Next article‘SERIKALI HAITAKUWA KIKWAZO KWA WAWEKEZAJI SEKTA YA VIWANDA’-WAZIRI JAFO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here