Featured Kitaifa

WANACHAMA 204 WALIOKIMBIA CUF WAREJEA

Written by mzalendoeditor

 Chama Cha Wananchi (CUF) kimewapokea wanachama 204 waliorudi wakitokea vyama vingine.

Miongoni mwa wanachama hao waliotambulishwa kutoka CCM, Chadema na ACT Wazalendo, 133 ni kutoka Tanzania Bara na 71 kutoka visiwani Zanzibar.

Akizungumza  katika hafla ya kuwakaribisha wananchama hao iliyofanyika Makao makuu ya chama hicho Buguruni jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba amesema watapangiwa majukumu ya kukijenga chama hicho.

“Nawashukuru kwa kurudi nyumbani sehemu ambayo haki inapiganiwa na nitoe wito kwa wengine warejee CUF, waje washike nafasi za uongozi hasa Zanzibar.

“Wengine hasa mimi umri wangu umeshakwenda, tunahitaji vijana waje waunganishe nguvu kuendelea mapambano ya kupigania haki sawa kwa wote,” amesema Profesa Lipumba.

Amesema chama hicho kinahitaji vijana kuziba nafasi mbalimbali kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa 2025 na kudai tume huru na Katiba mpya.

About the author

mzalendoeditor