Featured Kimataifa

ALIYEFUNGA NDOA NA WANAWAKE 17 AKAMATWA

Written by mzalendoeditor
Idadi ya wake katika orodha ya mzee wa Odisha nchini India mwenye umri wa miaka 66, ambaye alioa wanawake wa makamo, wasomi na matajiri wa majimbo mbalimbali, imeongezeka na kufikia 17 huku kesi tatu zaidi zikiibuka.

Hapo awali ilidaiwa kuwa mwanamume huyo ambaye kwa sasa yuko chini ya ulinzi wa mahakama, alikuwa ameoa mara 14.

Afisa wa polisi alisema mshtakiwa,aliyewadanganya wanawake kwa utambulisho bandia kuwa yeye ni daktari, pia alikuwa amefunga ndoa na daktari kutoka Assam na mwanamke mwenye elimu ya juu Odisha.

Kulingana na polisi, wanne kati ya wake zake hao wanaishi Odisha, watatu wapo Delhi, watatu Assam, wawili kila mmoja Madhya Pradesh na Punjab, na wengine wanaishi Chhattisgarh, Jharkhand na Uttar Pradesh.

CHANZO:BBCSWAHILI

About the author

mzalendoeditor