Featured Kitaifa

HOSPITALI YA AGA KHAN YAFANYA UPANDIKIZAJI UUME KWA MARA YA KWANZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI

Written by mzalendoeditor

Hospitali ya Chuo Kiku cha Aga Khan imesema imefanikisha upandikizaji wa kwanza wa uume katika kanda ya Afrika mashariki na kati .

Upasuaji huo maalum umefanyiwa kwa mwanaume katika umri wa miaka ya 40 ambaye alikuwa na hali ya maumbile nyeti kushindwa kuwa tayari, kwa kitaalamu Erectile dysfunction (ED) tatizo ambalo limemsumbua kwa miaka kadhaa kulingana na taarifa ya hospitali hiyo .

Tatizo hilo hutokea wakati ambapo mwanaume hawezi kushiriki katika tendo la ndoa kwa dakika 15 mfululizo na mgonjwa huyo alikuwa amepokea aina nyingine za matibabu bila hali yake kuboreka .

‘Upandikazaji huu huchukua takribai saa moja na unahusisha kuweka kifaa maalumu (Prosthesis) ambacho kinapachikwa kwenye uume na kumwezesha mtu kufanya tendo la ndoa wakati wowote bila kuhitajika kutumia dawa nyingine’ amesema Dkt.Ahmed Yousef aliyeongoza upasuaji huo .

Upasuaji huo umefanyika kwa mara ya kwanza katika ukanda huu kwa sababu unahitaji utaalamu wa kipekee na ufahamu wa kitengo cha tiba ya Urolojia.

Inakadiriwa kuwa asilimia 15-20 ya wanaume wana matatizo ya Erectile dysfunction (ED) na mshindo wa mapema(Premature Ejaculation) na wengi wanateseka kimya kimya kwa sababu ya hali hizo .

CHANZO:BBCSWAHILI

About the author

mzalendoeditor