Featured Michezo

DKT.TULIA AZINDUA KADI MPYA ZA UANACHAMA ZA KIELEKTRONIKI ZA YANGA,AITAKA KUWA NA MIPANGO ZAIDI

Written by mzalendoeditor

Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson , akimkabidhi Waziri ofisi ya Rais Kazi Maalum Mhe. Cpt. George Mkuchika kadi namba moja ya uanachama ya kielektroniki kwa klabu ya Yanga katika hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika leo katika hoteli ya Nashera Jijini Dodoma, Februari 18, 2022

Waziri ofisi ya Rais Kazi Maalum Mhe. Cpt. George Mkuchika akimkabidhi jezi ya Klabu ya Yanga Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), katika hafla fupi ya uzinduzi wa kadi mpya ya uanachama ya kielektroniki ya klabu ya Yanga iliyofanyika leo katika hoteli ya Nashera Jijini Dodoma, Februari 18, 2022

 Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson , akizungumza na viongozi wa Klabu ya Yanga na Wabunge wapenzi wa Yanga katika hafla fupi ya uzinduzi wa kadi mpya ya uanachama ya kielektroniki ya klabu ya Yanga iliyofanyika leo katika hoteli ya Nashera Jijini Dodoma, Februari 18, 2022, Kuanzia kushoto ni Mkurugenzi wa uwekezaji wa Klabu ya Yanga, Injinia Hersi Said, Meneja wa timu ya Bunge Sports Club, Mhe. Seif Gulamali , Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Yanga, Ndg. Senzo Mazingiza na Waziri ofisi ya Rais Kazi Maalum Mhe. Cpt. George Mkuchika 

Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson , katika picha ya pamoja na viongozi wa Klabu ya Yanga na Wabunge wapenzi wa Yanga katika hafla fupi ya uzinduzi wa kadi mpya ya uanachama ya kielektroniki ya klabu ya Yanga iliyofanyika leo katika hoteli ya Nashera Jijini Dodoma, Februari 18, 2022, Watatu kushoto mbele ni Waziri ofisi ya Rais Kazi Maalum Mhe. Cpt. George Mkuchika, Mwenyekiti wa timu ya Bunge Sports Club, Mhe. Tarimba Abbas (kulia mbele), na Meneja wa timu ya Bunge Sports Club, Mhe. Seif Gulamali (wapili

…………………………………………………….

Na.Alex Sonna,DPDOMA

Spika wa Bunge Dk.Tulia Akson amezindua kadi mpya za uanachama za Kieletroniki za Klabu ya Yanga  kwa Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku  akiitaka  kuweka mipango ya kutafuta  wachezaji wenye vipaji kutoka katika ligi ndogondogo na wale wanaotoka mitaani.

Uzinduzi wa Kadi za Kieletroniki ni sehemu ya mchakato wa mabadiliko ya Kidigital na mfumo wa uendeshaji wa Klabu kwa mujibu wa Katiba ya Yanga toleo la 2021.

Akizungumza leo Februari 18,2022,wakati wa uzinduzi huo,uliohudhuriwa na wanachama wabunge wa timu hiyo,wakiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa timu hiyo ambaye pia ni Waziri Ofisi ya Rais Ikulu kazi maalum  George Mkuchika Spika Tulia amesema kuna haja ya Klabu hiyo kuvisaidia vipaji ambavyo vipo mitaani.

Amesema anatamani kuona  wachezaji kutoka katika Ligi ndogondogo wanapewa nafasi ya kuzichezea Klabu kubwa huku akiwataka viongozi kutuma wawakilishi wakati zikichezwa ligi ili waweze kupata wachezaji wazuri.

“Kwahiyo mimi natamani viongozi katika hatua zile ambazo mnaendelea nazo basi muweke mipango mahususi kwa ajili ya hizi ligi ndogo ndogo zinazokuwa maeneo mbalimbali au hizi Cup ndogo ndogo mkisia Cup mahali basi mtume hata mwakilishi saa zingine si kocha,kocha ni mtu mkubwa.

Wale watu wenu kule Mikoani hii si timu ya Wananchi mpo kila mahali wawe wanahudhuria maeneo ili wale wachezaji wadogo wanaocheza kule waweze kuonekana na waje katika Klabu kubwa kama hii na inaweza kuwachukua na kuanza kuwalea kwa sababu tunatamani na sisi tuwe na majina makubwa makubwa.

“Kama hayo ambayo tunayasikia kwingine na hatutaweza kupata hayo majina makubwa kama Klabu kama Yanga haitawatafuta hao vijana na kaunza kuwalea  na wapo wale wanaohitaji  kulelewa kidogo tu na tutawapata kule mtaani,”amesema.

Pia,Spika Tulia ameitaka timu hiyo kukekemea kwa nguvu zote vurugu michezoni ambazo zimekuwa zikifanywa na baadhi ya mashabiki ambao huwa wanaingia viwanjani kwani michezo ni furaha na undugu.

Naye,Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya ufundi wa timu hiyo,Dominick Albinus amesema ni tukio hilo ni mwanzo wa wanawachama waliojiandikisha kuanza kupata kadi zao ambapo ndani ya wiki mbili wanachama wengine wataanza kupata kadi zao katika matawi yao.

Kwa upande wake,Mwenyekiti wa Tawi la Yanga Bungeni,Seif Gulamali ambaye ni Mbunge wa Manonga amesema zaidi ya wabunge 120 ambao ni wanachama wa yanga wamejisajili kupata kadi hizo wakiwemo baadhi ya Mawaziri na Naibu Waziri

About the author

mzalendoeditor