Featured Kitaifa

IGP SIRRO AITAKA JAMII KUACHA KUJIHUSISHA NA VITENDO VYA UNYANYASAJI

Written by mzalendoeditor

DAR ES SALAAM

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro ameitaka jamii kuacha kujihusisha na vitendo vya unyanyasaji wa Kijinsia na watoto pamoja na kuachana na mila potofu zilizopitwa na wakati na zinasosababisha madhara kwa jamii ikiwemo ukeketaji.

IGP Sirro amesema hayo wakati akipokea msaada wa Pikipiki Kumi (10) zilizotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu Duniani – UNFPA mahususi kwa ajili ya Ofisi za Dawati la Jinsia na Watoto  katika Mikoa ya Mara, Tarime Rorya, Kigoma na Makao Makuu ya Polisi.

Wakati huo huo IGP Sirro amekemea vitendo vya ukeketaji, ubakaji na udhalilishaji vinavyofanywa kwa watoto wadogo huku baadhi ya watu wengine wakifanya vitendo hivyo kama mradi wa kuwaingizia kipato.

Naye Mwakilishi wa  Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu Duniani – UNFPA Georgette Kyomba, ameitaka jamii kuacha kujihusisha na vitendo ya ukatili wa kijinsia.

About the author

mzalendoeditor