Kimataifa

SERIKALI YAANZISHA ENEO MAALUM LA UWEKEZAJI LA EPZA JIJINI DODOMA KWA AJILI YA KUJENGA KONGANI ZA VIWANDA

Written by mzalendo

 

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashantu Kijaji akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Athony Mtaka wakikagua eneo maalum la uwekezaji (SEZ) lenye ukubwa wa hekari 1500 katika eneo la viwanda Nala lililotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uwekezaji na Mauzo ya Nje (EPZA), iliyofanyika jijini Dodoma.

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashantu Kijaji ,akipata maelezo kutoka kwa Ofisa Mipango miji wa Halmashauri ya jiji la Dodoma, Aisha Masanja kuhusu ujenzi wa Kongani ya Viwanda katika eneo la viwanda Nala lililotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uwekezaji na Mauzo ya Nje (EPZA), iliyofanyika jijini Dodoma.

 

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashantu Kijaji,akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya eneo maalum la uwekezaji (SEZ) lenye ukubwa wa hekari 1500 katika eneo la viwanda Nala lililotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uwekezaji na Mauzo ya Nje (EPZA), iliyofanyika jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara  Prof.Godius Kahyarara ,akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya eneo maalum la uwekezaji (SEZ) lenye ukubwa wa hekari 1500 katika eneo la viwanda Nala lililotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uwekezaji na Mauzo ya Nje (EPZA), iliyofanyika jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Athony Mtaka,akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya eneo maalum la uwekezaji (SEZ) lenye ukubwa wa hekari 1500 katika eneo la viwanda Nala lililotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uwekezaji na Mauzo ya Nje (EPZA), iliyofanyika jijini Dodoma.

……………………………………………………..

Na.Alex Sonna,Dodoma.
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashantu Kijaji  amesema Serikali imeanzisha Kongani ya Viwanda Dodoma itakayokuwa na viwanda vitakavyotumia malighafi zinazozalishwa hapa nchini, ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya   Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan katika uanzishaji wa kongani za viwanda.

Dkt Kijaji ameyasema hayo katika Hafla fupi ya makabidhiano ya eneo maalum la uwekezaji (SEZ) lenye ukubwa wa hekari 1500 katika eneo la viwanda Nala lililotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uwekezaji na Mauzo ya Nje (EPZA), iliyofanyika jijini Dodoma Januari 20, 2022.

“Kongani hii  itumike kuhudumia Kanda ya kati kwa kuwa na  viwanda vya kuchakata mazao ya kilimo hususan Alizeti inayolimwa Dodoma, Singida na Simiyu ili kuwa na mafuta ya kula ya kutosha mahitaji ya ndani na  kuuza nje ya nchi na kutumia Reli ya Kisasa ya SGR kwa kusafirisha mizigo kwenda masoko ya nje ya nchi.” Amesema Waziri Kijaji.

Waziri Kijaji pia amezielekeza Taasisi za EPZA na TIC kushirikiana na Sekta Binafsi pamoja na Uongozi wa Mkoa wa Dodoma ili kuhakikisha kongani hiyo inaendelezwa kwa wakati ili kutimiza malengo ya Serikali ya Awamu ya Sita katika uanzishaji, uendelezaji na uwekezaji wa kongani za viwanda nchini.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka amebainisha Maeneo ya EPZA yanavutia wawekezaji hivyo Ofisi yake iko tayari kushirikiana na Wizara katika kuhakikisha miundombinu muhimu kama Maji, Umeme na Barabara inapatikana ili kukamilisha ujenzi wa kongani hiyo kwa wakati na kuvutia wawekezaji  na hivyo kuleta maendeleo katika mkoa huo na kwa Taifa.

”Tunataka  Rais Samia Suluhu Hassan akifikisha mwaka mmoja Machi 17 kama mkoa tumueleze  nini kimefanyika na akifikisha miaka 10 wamweleze nini kimefanyika eneo la uwekezaji wa viwanda.

Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara  Prof.Godius Kahyarara amesema ni muhimu EPZA kutenga maeneo ya kongani za kiuchumi  zenye hadhi ya kimataifa kwa kuzingatia wawekezaji wadogo zinazolenga kutoa ajira nyingi ili kutimiza Malengo ya Serikali katika kuongeza ajira na pato la Taifa.

” EPZA tengeni kongani maalum kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vya uzalishaji bidhaa za ujenzi ili kutosheleza mahitaji ya vifaa hivyo nchini ili tusiwe  tunaagiza vifaa hivyo kutoka nje ya nchi. 

Awali akiongea, Mkurugenzi Mkuu wa EPZA Bw. Charles Itembe amesema eneo hilo lililotengwa linatarajiwa kuwa kitivo maalumu cha uwekezaji katika nyanja mbali mbali kama vile  ununuzi,usafirishaji, kilimo, ujenzi, madinj, nguo na madawa na litatoa ajira takriban 100,000.

Naye, Afisa Mipango wa mkoa wa Dodoma amebainisha kuwa Mkoa umetenga maeneo kwa ajili ya ujenzi wa viwanda ambapo katika eneo la Nala hekari 2285 ambapo hadi sasa hekari 300 zimegawiwa kwa wawekezaji wa nje, 1500 kwa EPZA, na 21 kwa wawekezaji wazawa.

About the author

mzalendo