katibu mkuu wa Taasisi ya utaalamu wa utawala Tanzania(APAT) Mhe. Christopher Kabalika akiongea na waandishi wa habari katika mkutano huo.
Afisa utumishi wa manispaa ya Temeke Bihaga Yogwa alieleza jambo katika mkutano wa APAT.
Muhadhiri kutoka chuo kikuu cha Mzumbe Dkt Venance Shillingi akiongea na waandishi wa habari katika mkutano huo.
Baadhi ya maafisa utumishi na mafisa rasilimali watu wakifuatilia jambo katika mkutano wao unaoendelea mkoani Arusha.
……………………………………………….
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA
Taasisi ya utaalamu wa utawala Tanzania(APAT) imewakutanisha maafisa rasilimali watu na watawala zaidi ya 500 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania mkoani Arusha katika mkutano wao wa kimataifa wenye lengo la kujadili mustakabali wa kuunganisha vyama vya watawala na vyama vya rasilimali watu ili kuona namna ya kuunda bodi itayokuwa inasimamia masuala ya pande zote mbili.
Akiongea na waandishi wa habari katika mkutano wao ulioanza leo May 18, 2022 katibu mkuu wa taasisi hiyo Mhe. Christopher Kabalika alisema kuwa wanataka wawe na chama kimoja kikubwa, chenye nguvu ambacho kitaweza kubeba maana ya watawala na rasilimali watu kujua nini kinafanyika katika taifa.
“Lakini pia tutajadili namna gani tutaweza kuunda bodi ya maafisa rasilimali watu na watawala Tanzania ili mambo yetu yote yaweze kupitia kwenye bodi hiyo kwaajili ya kudhibidi na kujua nini tutafanya kama ilivyo katika bodi zingine zinazosimamia taaluma mbalimbali,”Alisema Mhe.Kabalika.
Alifafanua kuwa mkutano huo ni wa siku tatu ambapo watajadili agenda mbalimbali na siku ya mwisho wanatarajia utafungwa na waziri wa utumishi na utawala bora Jenista Muhagama ambapo wameiomba serikali kuangalia kiumakini iwe weweze kupata bodi.
Kwa upande wake Afisa utumishi manispaa ya Temeke Bihaga Yogwa alieleza kuwa Kuna changamoto ya kutokuwa na bodi katika tasnia hiyo kwani wanakosa chombo kimoja kinachosimamia mambo yao lakini wakipata bodi watakuwa imara na wenye nguvu zaidi katika kushughulika na masuala yao.
Naye muhadhiri kutoka chuo kikuu cha Mzumbe Dkt Venance Shillingi alisema kuwa watakapo unganisha kada hizo mbili itawafanya wawe na nguvu itakayoshawishi serikali wawe na bodi ya kuwasimamia kwani wakiwa na bodi hiyo kada hizo zitakiwa na ambavyo mpaka mtu awe navyo ndipo aweze kuwa afisa utumishi au afisa utawala.
“Kazi ya afisa utumishi sio kuajiri tu na kufukuza bali ni mtu pekee ambaye anaweza kufanya taasisi ikafanya vizuri kuliko kada nyingine yoyote na hii itafanya afisa utumishi awe ni sehemu ya taasisi kwa kujua taasisi ina mikakati gani kwa miaka ijayo aweze kusaidiabkupata wafanya wenye sifa stahiki ya kutekeleza hiyo mikakati,”Alisema Dkt Shillingi.
Alisema kuwa wakishaunganisha nguvu na kitu kimoja watakuwa na matawi mawili moja la maafisa utumishi na lingene utawala lakini kwa juu wanakuwa timu moja ili watakapokuwa na hoja yoyote waweze kusikilizwa.