Featured Kitaifa

TBS YAWAKUMBUSHA WABUNIFU KUSAJILI KAZI ZAO

Written by mzalendoeditor

Afisa Usalama wa chakula kutoka  TBS Kanda ya Kati,Sifa Chamgenzi akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea Banda la TBS  wakati wa  maonesho ya wiki ya ubunifu yanayokwenda sambamba na Mashindano ya Ubunifu wa Sayansi na Teknolojia (MAKISATU) kwa mwaka 2022 ambayo yameandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo(UNDP) kupitia mradi wake wa FUNGUO yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Afisa Udhibiti Ubora kutoka  TBS Kanda ya Kati,Sileja Lushibika,akiwaeleza wananchi waliofika kwenye Banda la TBS kuhusu kazi zinazofanywa na shirika hilo wakati wa  maonesho ya wiki ya ubunifu yanayokwenda sambamba na Mashindano ya Ubunifu wa Sayansi na Teknolojia (MAKISATU) kwa mwaka 2022 ambayo yameandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo(UNDP) kupitia mradi wake wa FUNGUO yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

……………………………………

Na Alex Sonna _DODOMA 

SHIRIKA la Viwango nchini (TBS)  limewaomba wajasiriamali kufika katika Banda  la Shirika hilo lilopo katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma kwa lengo la kwenda kuthibitisha bidhaa zao kwani kufanya hivyo ni bure.

Hayo yameelezwa leo Mei 17,2022 na  Afisa Usalama wa chakula kutoka  TBS Kanda ya Kati,Sifa Chamgenzi wakati akizungumza na akiwa kwenye banda la Shirika hilo kwenye maonesho ya wiki ya ubunifu yanayokwenda sambamba na Mashindano ya Ubunifu wa Sayansi na Teknolojia(MAKISATU) kwa mwaka 2022 ambayo yameandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo(UNDP) kupitia mradi wake wa FUNGUO yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Chamgenzi amesema wapo kwa ajili ya kuangalia wajasiriamali ambao wamebuni kazi mbalimbali na kuzisajili ambapo amedai zoezi hilo wanalifanya  bure.

“Tunawakaribisha sana kwa ajili ya kupata nembo  ya ubora ukiwa kama mjasiriamali unapewa na unatumia kwa miaka mitatu bure  hulipiii chochote mwaka wa nne ndio utaanza kulipia,”amesema.

Kwa upande wake,Afisa Udhibiti Ubora kutoka  TBS Kanda ya Kati,Sileja Lushibika amewataka wajasiriamali  mbalimbali nchini kuzipeleka kazi zao ili ziweze kuwa na ubora wa kushindana katika masoko ya nje.

“Sisi kama TBS tunategemea tuone huo ubunifu  halafu tukaseme huo ubunifu uende na viwango kwani unabuni ili kitu kiende mbali sana.

“Huwezi kuuza kitu sokoni kama hakina ubora tunashauri baada ya kufanya ubunifu tunawapa ushauri ili tuipe thamani  zaidi  bidhaa yako.Kama wataweza kuja kwetu watakuwa na uwezo wa kushindana na soko la nje,”amesema.

Amesema  kwa wale wanaotembelea banda lao  wamewapa  elimu kuhusu TBS huku wakidai wajasiriamali ndio ambao wamekuwa wakipewa kipaumbele.

“Ili uweze kupata alama ya ubora hasa kwa mjasiriamali tunapenda kuwatangazia kwamba watapata alama za ubora kwa muda wa miaka mitatu sharti lazima awe na leseni awe anatambulika na Sido pamoja na ni raia wa Tanzania,”amesema

Amesema wamekuwa pia wakitoa elimu kwa watanzania jinsi ya kutumia vipodozi kwani kuna vingine vina madini yenye sumu na ni kwa ajili ya matumizi ya dawa.

Naye,Besther Mseluka Mkazi wa Ilazo ambaye alifika katika banda hilo, amesema ni vema watu wakafika katika banda hilo ili waweze kupata elimu juu ya matumizi ya vipodozi.

“Ninashukuru kwenye hili banda nimejifunza kumbe kuna mafuta hatutaki kuyatumia kwa sababu yanaleta kansa, afya ni namba moja kuliko kitu chochote.Nje tutaonekana ni wazuri lakini ndani kuna matatizo,”amesema.

About the author

mzalendoeditor