PICHA mbalimbali za Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwa katika mkutano wake wa hadhara wa kampeni uliofanyika leo Oktoba 15,2025 katika kata ya Puma wilaya ya Ikungi ndani ya Jimbo la Ikungi Magharibi mkoani Singida.
Akiwa Katika mkutano huo,Dkt.
Nchimbi aliinadi Sera na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya 2025-2030 kwa Wananchi ikiwemo na kuwaomba kumpigia kura za ushindi wa kishindo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Dkt.Samia Suluhu Hassan,Wabunge na Madiwani.
Aidha,Dkt Nchimbi pia alitumia nafasi hiyo kuwanadi baadhi ya wagombea Ubunge wa mkoa huo akiwemo mgombea Ubunge wa jimbo la Ikungi Magharibi Ndugu Elibariki Immanuel Kingu,mgombea Ubunge jimbo la Ikungi Mashariki Ndugu Thomas Mgonto KITIMA na Madiwani.
Balozi Nchimbi anafikia mkoa wa 23 sasa tangu kuzinduliwa kwa kampeni hizo Agosti 28,2025 jijini Dar es Salaam,akiendelea kusaka kura za ushindi wa kishindo za mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi,Dkt.Samia Suluhu Hassan,Wabunge na Madiwani.