Featured Kitaifa

DKT NCHIMBI ASIMIKWA KIMILA KUWA ‘MTONGI’ MSAIDIZI WA MTEMI, APEWA JINA LA ‘NYUNGU YA MAWE’.

Written by Alex Sonna

Mgombea mwenza wa kiti cha Uraisi kupitia chama cha mapinduzi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amesimikwa kuwa msaidizi wa Mtemi, kimila akiitwa ‘MTONGI’ baada ya mkubwa wake mtemi Hangaya ambaye ni Raisi Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Dkt. Nchimbi amesimikwa na viongozi wa kimila wa Unyanyembe (Tabora) kwenye mkutano wake wa mwisho wa kampeni mkoani humo,katika kata ya Kigwa jimbo la Igalula, wilaya ya Uyui nakupewa jina la “NYUNGU YA MAWE”.

About the author

Alex Sonna