Featured Kitaifa

DKT NCHIMBI “UZALISHAJI MAJI ‘ILALA’ KUFIKIA LITA MILIONI 845” | AHIMIZA WANANCHI KUTIKI IFIKAPO OKTOBA 29

Written by Alex Sonna

Mgombea mwenza wa kiti cha Urais kupitia CCM, Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi amesema kwamba Serikali ijayo ya Dkt. Samia Suluhu Hassan imenuia kwa dhati kuongeza uzalishaji wa Maji katika Wilaya ya Ilala kutoka ujazo wa lita takribani M
milioni 273 hadi kufikia ujazo wa lita milioni 845.

Dkt Nchimbi ametoa kauli hiyo leo Septemba 30, 2025 Jijini Dar es Salaam katika Jimbo la Ukonga, Wilaya ya Ilala katika mwendelezo wa mikutano ya K
kampeni za Urais kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29 mwaka huu.

“Nataka niwaambie ndugu zangu wana Ilala, hiyo ndio ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya 2025-2030 ilivyojipanga kuondoa changamoto ya maji kwa Wakazi wa Ilala na Vitongoji vyake katika majimbo ya Ukonga na Segerea, ambapo Ongezeko hilo ni zaidi ya mara nne, kwa hiyo niwaombe tuendelee kuiunga mkono CCM ili iweze kutimiza ahadi zake kwa wananchi” amesema Dkt Nchimbi.

About the author

Alex Sonna