Featured Kitaifa

DK.NCHIMBI:SERIKALI YA CCM KURASIMISHA BIASHARA ZA WAJASIRIAMALI WADOGO

Written by Alex Sonna

Mgombea mwenza wa urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amesema serikali ijayo ya CCM imejipanga kwa dhati kurasimisha biashara za wafanyabiashara wadogo ili kuongeza tija na kukuza kipato cha wananchi.

Akihutubia wananchi katika eneo la EPZA-Mabibo, Wilaya ya Ubungo, Dar es Salaam leo jSeptemba 29, 2025, Dkt. Nchimbi amesema kuwa  utekelezaji wa sera na Ilani ya CCM ya mwaka 2025–2030 utalenga kuimarisha shughuli za kiuchumi na kupeleka maendeleo kwa Watanzania.

Aidha, baada ya mkutano huo, ametumia nafasi hiyo kuwanadi baadhi ya wagombea wa CCM mkoani humo, akiwemo Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Prof. Kitila Mkumbo, pamoja na madiwani wa kata mbalimbali.

Dkt. Nchimbi ni mgombea mwenza wa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025, ambapo Dar es Salaam unakuwa  mkoa wa 15 kufikiwa na kampeni zake za kuomba ridhaa ya wananchi kwa ajili ya ushindi wa CCM katika nafasi ya urais, ubunge na udiwani.

About the author

Alex Sonna