Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Mhandisi Enock Nyanda akizungumza na wajumbe wa kikao kazi cha kikao kazi cha wadau na washauri washauri walekezi wa Mradi wa Mabadiliko ya Tabianchi wa UNCDF- LoCAL wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya matokeo ya tathmini ya Kitaifa ya Maeneo yenye Hatari na Uwezekano wa Kuathirika kutokana na Mabadiliko ya Tabianchi (CRVA) Jijini Dodoma Septemba 24, 2025.
NaMwandishi Wetu- DODOMA
OFISI ya Rais- TAMISEMI imezindua matokeo ya tathmini ya Kitaifa ya Maeneo yenye Hatari na Uwezekano wa Kuathirika kutokana na Mabadiliko ya Tabianchi.
Taarifa ya matokeo ya tatmini hiyo imefanywa na Shirika la Mitaji ya Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNCDF) kupitia Programu ya LoCAL kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya, Serikali ya Norway, Ubelgiji na Ireland.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa matokeo ya tathmini hiyo leo Septemba 24, 2025 Jijini Ddoma, Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Mhandisi Emmanuel Nyanda amesema matokeo hayo yamewasilishwa katika ngazi ya halmashauri za Tanzania Bara na Zanzibar.
Mhandisi Nyanda amesema Matokeo ya tathmini hii yatawawezesha watunga sera, viongozi wa halmashauri, na wananchi kupanga na kutekeleza hatua madhubuti za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
“Tunawashukuru UNCDF na, Umoja wa Ulaya,Norway, Ubelgiji, na Ireland, kwa kuunga mkono juhudi za serikali katika kutambua maeneo hatarishi na kuainisha mbinu za ustahimilivu“ amesema Mhandisi Nyanda.
Ameongeza kuwa Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa za mabadiliko ya tabianchi, ikiwemo ongezeko la joto, ukame, mafuriko na hivyo kuhitaji uwekezaji wa haraka na wa kimkakati ili kujenga ustahimilivu wa jamii.
Kuhusu Mradi wa LOCAL, Mhandisi Nyanda amesema mradi huo ulioanza kutekelezwa mwaka 2017 katika Halmashauri za Chamwino, Kondoa na Mpwapwa umeleta mafanikio makubwa katika afua za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi katika ngazi za msingi.
Ameeleza kufuatia mafanikio hayo, katika awamu ya pili ya utekelezaji wa mradi huo, UNCDF imepanga kupanua wigo wa utekelezaji kutoka Halmashuri tatu hadi kufikia halmashauri nane nchini.
Amezitaja Halmashauri zitakazonufaika na awamu ya pili ya Mradi wa UNCDF-LoCAL kywa ni Mkinga (Tanga), Mtama (Lindi), Kigamboni (Dar es Salaam), Mafia (Pwani) na Mtwara (Mtwara).
Kwa upande wake, Mratibu wa Mradi wa UNCDF-Local Tanzania, Bi. Aine Mushi, amesema Ripoti hiyo inatoa maarifa ya kisayansi, na UNCDF kupitia program ya LoCAL itaendelea kujengea uwezo Halmashauri ili kujenga ustahimilivu wa jamii.
“Tutahakikisha kila shilingi inayotumika katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi inafika kwa jamii zilizo hatarini zaidi, na kulinda mustakabali wa taifa kijamii na kiuchumi” amesema Bi. Mushi.
Aidha amesema Shirika la UNCDF limeendelea kupata ushirikiano kutoka kwa Serikali hususani kutoka katika Halmashauri za Wilaya zinazotekeleza mradi huo ambao umeleta manufaa kwa jamii.
Naye Mwakilishi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Sanford Kway amelishukuru Shirika la UNCDF kwa kuendelea kushirikiana na serikali katika kutatua changamoto za mabadiliko ya tabianchi katika maeneo mbalimbali nchini.
Mradi wa LoCAL unaotekelezwa na Shirika la UNCDF linafanya kazi pamoja na serikali kupitia OR-TAMISEMI na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa ajili ya kujengea uwezo jamii kupitia Mamlaka za Serikali za Mitaa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Mmoja wa wajumbe wa kikao kazi cha wadau na washauri elekezi Mradi wa Mabadiliko ya Tabianchi wa UNCDF- LoCAL, Bi. Salvata Silayo kutoka Wizara ya Afya akichangia mada wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya matokeo ya tathmini ya Kitaifa ya Maeneo yenye Hatari na Uwezekano wa Kuathirika kutokana na Mabadiliko ya Tabianchi (CRVA) Jijini Dodoma Septemba 24, 2025.
Mmoja wa wajumbe wa kikao kazi cha wadau na washauri elekezi wa Mradi wa Mabadiliko ya Tabianchi wa UNCDF- LoCAL, Dkt. Elisei Lubuva kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo akichangia mada wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya matokeo ya tathmini ya Kitaifa ya Maeneo yenye Hatari na Uwezekano wa Kuathirika kutokana na Mabadiliko ya Tabianchi (CRVA) Jijini Dodoma Septemba 24, 2025.
Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Mhandisi Enock Nyanda akizungumza na wajumbe wa kikao kazi cha kikao kazi cha wadau na washauri washauri walekezi wa Mradi wa Mabadiliko ya Tabianchi wa UNCDF- LoCAL wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya matokeo ya tathmini ya Kitaifa ya Maeneo yenye Hatari na Uwezekano wa Kuathirika kutokana na Mabadiliko ya Tabianchi (CRVA) Jijini Dodoma Septemba 24, 2025.Baadhi ya wajumbe wa kikao kazi cha cha wadau na washauri elekezi wa Mradi wa Mabadiliko ya Tabianchi wa UNCDF- LoCAL wakifuatilia majadiliano mbalimbali wakati wa kikao kazi cha mradi huo kilichofanyika Septemba 24, 2025 Jijini Dodoma ambacho kilipokea taarifa ya matokeo ya tathmini ya Kitaifa ya Maeneo yenye Hatari na Uwezekano wa Kuathirika kutokana na Mabadiliko ya Tabianchi (CRVA).Mratibu wa Mradi wa UNCDF-Local nchini Tanzania, Bi. Aine Mushi akizungumza na wajumbe wa kikao kazi cha wadau na washauri walekezi wa Mradi wa Mabadiliko ya Tabianchi wa UNCDF- LoCAL kilichofanyika Septemba 24, 2025 Jijini Dodoma wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya matokeo ya tathmini ya Kitaifa ya Maeneo yenye Hatari na Uwezekano wa Kuathirika kutokana na Mabadiliko ya Tabianchi (CRVA).
Baadhi ya wajumbe wa kikao kazi cha wadau na washauri elekezi wa Mradi wa Mabadiliko ya Tabianchi wa UNCDF- LoCAL wakifuatilia majadiliano mbalimbali wakati wa kikao kazi cha mradi huo kilichofanyika Septemba 24, 2025 Jijini Dodoma ambacho kilipokea taarifa ya matokeo ya tathmini ya Kitaifa ya Maeneo yenye Hatari na Uwezekano wa Kuathirika kutokana na Mabadiliko ya Tabianchi (CRVA).
Afisa Misitu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Sanford Kway akizungumza wakati wa kikao kazi cha wadau na washauri walekezi wa Mradi wa Mabadiliko ya Tabianchi wa UNCDF- LoCAL kilichofanyika Septemba 24, 2025 Jijini Dodoma ambacho kilipokea taarifa ya matokeo ya tathmini ya Kitaifa ya Maeneo yenye Hatari na Uwezekano wa Kuathirika kutokana na Mabadiliko ya Tabianchi (CRVA).
Baadhi ya Wajumbe wa kikao kazi cha wadau na washauri walekezi wa Mradi wa Mabadiliko ya Tabianchi wa UNCDF- LoCAL wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya ufunguzi wa kikao hicho Septemba 24, 2025 Jijini Dodoma ambacho kilipokea wa taarifa ya matokeo ya tathmini ya Kitaifa ya Maeneo yenye Hatari na Uwezekano wa Kuathirika kutokana na Mabadiliko ya Tabianchi (CRVA).
Afisa Misitu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Sanford Kway akizungumza wakati wa kikao kazi cha wadau na washauri walekezi wa Mradi wa Mabadiliko ya Tabianchi wa UNCDF- LoCAL kilichofanyika Septemba 24, 2025 Jijini Dodoma ambacho kilipokea taarifa ya matokeo ya tathmini ya Kitaifa ya Maeneo yenye Hatari na Uwezekano wa Kuathirika kutokana na Mabadiliko ya Tabianchi (CRVA).
Baadhi ya Wajumbe wa kikao kazi cha wadau na washauri walekezi wa Mradi wa Mabadiliko ya Tabianchi wa UNCDF- LoCAL wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya ufunguzi wa kikao hicho Septemba 24, 2025 Jijini Dodoma ambacho kilipokea wa taarifa ya matokeo ya tathmini ya Kitaifa ya Maeneo yenye Hatari na Uwezekano wa Kuathirika kutokana na Mabadiliko ya Tabianchi (CRVA).