Featured Kitaifa

MAELFU WAJITOKEZA MAKAMBAKO KUMSIKILIZA DKT.SAMIA

Written by Alex Sonna

MAKAMBAKO, NJOMBE 

Maelfu ya wananchi wamejitokeza leo Jumamosi Septemba 6, 2025, mjini Makambako, mkoani Njombe, kwa ajili ya kumsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye anaendelea na mikutano yake ya kampeni katika Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.

Wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Makambako na vijiji vya jirani walifurika kwenye soko kuu la Makambako, ambapo mkutano huo umefanyika , wakionesha hamasa kubwa kwa kujitokeza mapema asubuhi wakiwa na bendera na fulana za chama chake.

Katika mkutano huo, Dkt. Samia amewasilisha sera na vipaumbele vyake kwa wananchi, huku akisisitiza kuendeleza miradi ya maendeleo, kuboresha huduma za kijamii na kuimarisha uchumi wa wananchi wa kada zote.

Baada ya mkutano wa Makambako, Dkt. Samia anatarajiwa kuendelea na ratiba yake ya kampeni mkoani Iringa, ambapo atafanya mikutano mingine ya hadhara katika maeneo kadhaa ya mkoa huo.





About the author

Alex Sonna