Featured Kitaifa

BINTI ALIYETESEKA NA UVIMBE TUMBONI ATOLEWA UVIMBE WA KILO MBILI NA NUSU

Written by Alex Sonna

Na. Jeremiah Mbwambo, 24/07/2027 Bujumbura – Burundi

Daktari Bingwa wa Upasuaji Joseph Loth aliye mfanyia upasuaji amesema binti huyo amekuwa akipata maumivu makali yanayo kuja na kupotea

“Uvimbe huu tuliotoa ni uvimbe wa ukuta wa mbele wa utumbo (anterior abdominal wall tumour) ambao una kilo mbili na nusu” alisema Dkt. Loth

Ameongeza kuwa kama uvimbe huu usingetolewa ungemletea madhara zaidi na hata kupoteza maisha yake

“Kama uvimbe huu usinge tolewa ungeendelea kukuwa na matokeo yake ungekandamiza viongo vingine vya ndani ya tumbo kama kibofu, via vya uzazi (mayai na mfuko wa uzazi) na mishipa ya damu inayo shusha na kupandisha damu miguuni, uvumbe huu tulioutoa amekaa nao kwa zaidi ya miaka mitatu na ulikuwa ukiendelea kukua” amesema Dkt. Loth

Madaktari Bingwa wa Hospitali ya Benjamin Mkapa wameweka kambi katika Mkoa wa Bujumbura nchini Burundi.

About the author

Alex Sonna