KLABU ya Manchester United imejikuta ikiondoshwa mapema katika michuano ya Kombe la Carabao (EFL Cup) baada ya kufungwa kwa mikwaju ya penalti 12-11 dhidi ya Grimsby Town FC, timu inayoshiriki Ligi Daraja la Nne nchini England.
Katika mchezo huo wa raundi ya pili uliopigwa usiku wa kuamkia leo kwenye dimba la Blundell Park, Grimsby ilionesha upinzani mkali dhidi ya mashetani wekundu, na kusababisha matokeo ya sare ya 2-2 ndani ya dakika 90 za kawaida kabla ya kwenda kwenye penalti.
Baada ya dakika ya 90 kumalizika kwa sare ya kufungana mabao 2-2 zikaenda hatua ya Mikawaju ya Penalti ambapo Grimsby walitoka kidedea kwa ushindi wa 12-11 .