Featured Kitaifa

DK.BITEKO AAGIZA MINADA NCHINI KUTUMIA NISHATI SAFI KUCHOMEA NYAMA

Written by Alex Sonna

Na.Alex Sonna_DODOMA

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk.Doto Biteko, ameagiza minada yote nchini kuacha matumizi ya kuni na mkaa kwa ajili ya kuchoma nyama ili kulinda mazingira na afya za watuaji nishati hiyo chafu.

Dk.Biteko, ameyasema hayo leo Agosti 21,2025 wakati akizungumza na Mamalishe na Babalishe wanaofanya biashara kwenye Mnada wa Msalato jijini Dodoma, ikiwa ni sehemu ya uhamasishaji matumizi ya nisahti safi kwa wadau wa uchomaji nyama mnada wa Msalato.

Amesema kuwa , serikali ya Tanzania imeweka malengo kuwa ifikapo 2034, asilimia 80 ya Watanzania wote wawe wanatumia nishati safi ya kupikia.

Aidha Dk.Biteko amesema ili kufikia malengo hayo ni lazima kuanzia sasa maeneo ya minada kuanza matumizi ya nishati safi ya kupikia kama ilivyo kwa magereza,shule pamoja na meneo mengine yenye mikusanyiko.

“Nashukuru hivi sasa maeneo ya majeshi yetu shule na yale mengine yenye mikusanyiko kuanza kutumia nisahti ya kupikia lakini sasa ni wakati wa minada yote nchini kuanza magumizi ya nisahti Safi ya kupikia kwa ajili ya kuchoma nyama ili kulinda mazingira na afya za wafanyabishara wetu,”amesema Dk.Biteko

Hata hivyo ameliagiza Shirika la Taifa la Madini (STAMICO) kutafuta wakala ambaye atauza mkaa mbadala wanaouzalisha ili kuwasaidia wafanyabiashara wa kuchoma nyama kwenye mnada huo kuacha matumizi ya kuni na mkaa.

Pia ameuagiza wakala wa Nishati Vijijini(REA) kufunga Mariko yanayotumia mkaa huo mbadala ndani ya wiki mbili ili kuwezesha wafabiashara hao kuwa na maeneo maalum ya kuchoma nyama ambayo hayataathiri uasili wa eneo hilo.

“Watu wanakuja mnadani kuchoma nyama kwasababu ya upekee uliopo hapa kama usipoluwepo upee huo watu watakwenda hotelini kuchoma nyama hivyo yunavyoweka Mariko haya ya kuchoma nyama kwa mkaa mbadala lazima mazingira ya hapa yabaki yalivyo”amesema

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Nisahati Mhandisi Felchesm Mramba,  amesema kuwa ufungaji Majiko yanayotumia nisahti safi kwenye minada litafanyika katika mikoa yote nchini.

“Zoezi hili limenzia hapa Dodoma kama mwanzo tuu lakini liyakuwa endelevu na litakwenda kwenye mikoa yote nchini lengo ni kuunga mkono jiyihada za Rais Samia Suluhu Hassan kuhamasisha matumizi ya nisahti safi ya kupikia”,amesema

Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA) Hassan Said, amesema  kwa mujibu wa utafiti waliofanya asilimia 89.5 ya wachoma nyama waliolizwa kuhusu matumizi ya nisahti safi walisema hawatumi na asilimia 26.3 ndiyo wanatumia.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule  amesema walaji katika mnada wa Msalato kwa wiki ni kati ya 2000 na 3000 hivyo kwa kutumia Nishati Safi ya Kupikia itawezesha kuokoa mazingira kwa kuondokana na kuni na mkaa ambao ulikuwa ukitumika kuhudumia idadi hiyo ya watu. 
Aidha ameomba kampeni hiyo ya Nishati Safi ya Kupikia ifike kwenye masoko mbalimbali ambayo ina mama lishe na baba lishe.

 

About the author

Alex Sonna