TIMU ya Arsenal wameendeleza moto wa kuzichapa timu pinzania baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Leeds United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England uliopigwa Uwanja wa Emirates Jijini London.
Mabao yote ya Arsenal yamefungwa na Eddie Nketiah dakika ya tano na ya 10, wakati la Leeds limefungwa na Diego Llorente dakika ya 66.
Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 66, ingawa inabaki nafasi ya nne, ikizidiwa pointi moja na Chelsea baada ya wote kucheza mechi 35, wakati Leeds inabaki na pointi zake 34 za mechi 35 pia nafasi ya 18.