Featured Kitaifa

WATUMISHI WAPYA HANDENI MJI WATAKIWA KUZINGATIA MAADILI UTUMISHI WA UMMA

Written by Alex Sonna

 

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Mji Handeni, Maryam Ukwaju, akziungumza wakati WA mafunzo ya awali Kwa watumishi watumishi wapya wa halmashauri hiyo.

 

Na Mwandishi wetu, Handeni

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Mji Handeni, Maryam Ukwaju, amewataka watumishi wapya wa halmashauri hiyo kuzingatia taratibu, sheria na miongozo ya utumishi wa umma katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Akizungumza  wakati wa mafunzo ya awali kwa watumishi hao mjini Handeni, Ukwaju amesema ni wajibu wa kila mtumishi kuhakikisha anailinda heshima ya utumishi wa umma kwa kuepuka vitendo vinavyokwenda kinyume na maadili, ikiwemo kuomba au kupokea rushwa pamoja na tabia ya ulevi.

Amesisitiza kuwa mshikamano na ushirikiano miongoni mwa watumishi ni nyenzo muhimu ya kufanikisha utekelezaji wa majukumu na kuchochea maendeleo ya halmashauri hiyo.

Awali, Mkuu wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa halmashauri hiyo, Steven Bavu, amewataka watumishi hao kuwajibika kwa weledi na nidhamu ya kazi, akibainisha kuwa uzembe na kutojibidiisha ni miongoni mwa changamoto zinazopunguza tija katika sekta ya umma.

“Watumishi wengi tunajisahau na kushindwa kuwajibika ipasavyo. Ukiingia kazini usilale, jifunze muda wote ili kujiongezea ujuzi utakaokuletea tija katika utekelezaji wa majukumu yako,” amesema Bavu.

About the author

Alex Sonna