Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula akizungumza katika kikao baina ya Menejimenti ya Wizara hiyo na Shirika la UNFPA jijini Dodoma
Naibu Mwakilishi Mkaazi wa UNFPA Dkt. Wilfredy Ochan akieleza vipaumbele vya Shirika hilo mbele ya Menejimenti ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, katika kikao kati ya Wizara na Shirika hilo kilichofanyika jijini Dodoma
Baadhi ya Wakurugenzi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum wakifuatilia kikao cha Menejimenti ya Wizara hiyo na Shirika la UNFPA wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula, jijini Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula akiagana na Naibu Mwakilishi Mkaazi wa UNFPA Dkt. Wilfredy Ochan mara baada ya mazungumzo baina ya Wizara na Shirika hilo yaliyofanyika jijini Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Mwakilishi Mkaazi wa UNFPA Dkt. Wilfredy Ochan (wa tatu kushoto) mara baada ya mazungumzo baina ya Wizara na Shirika hilo yaliyofanyika jijini Dodoma Mei 07, 2022.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WMJJWM
………………………………………………………………
Na WMJJWM- Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Zainab Chaula amekutana na Ujumbe kutoka Shirika la UNFPA ukiongozwa na Naibu Mwakilishi Mkaazi wa UNFPA Dkt. Wilfredy Ochan.
Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika Mei 07, 2022 jijini Dodoma Dkt. Chaula amesema Wizara inaendelea kukutana na wadau mbalimbali kwa lengo la kuweka vipaumbele na mikakati ikiwemo ya kuwawezesha Wanawake kiuchumi na Usawa wa Kijinsia.
Ameongeza kuwa Wizara imejipanga katika kuboresha Sera, Mipango na mikakati mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha jamii inanufaika nayo hasa katika kupambana na vitendo vya ukatili, uwezeshaji wa Wanawake kiuchumi, Usawa wa Kijinsia, Ustawi wa Wazee na Watoto.
Kwa upande wake Naibu Mwakilishi Mkaazi wa UNFPA Dkt. Wilfredy Ochan alisema Shirika hilo lipo tayari kushirikiana na Wizara katika kuhakikisha Sera, Mipango na Mikakati iliyopo inawezeshwa na kuleta matokea chanya kwa jamii na maendeleo ya Taifa.
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum inaendelea kukutana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha kuwa inaweka mikakati inayolenga kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.