Featured Kitaifa

MRADI WA SEQUIP WAPELEKA NEEMA MKOANI GEITA

Written by mzalendoeditor

Kupitia Mradi wa kuboresha Ubora wa Elimu Sekondari (SEQUIP) wananchi mkoani Geita wamenufaika na miundombinu ya ujenzi wa shule mpya mbili za sekondari zitakazorahisisha upatikanaji wa huduma za elimu mkoani humo.

Shule hizo ni pamoja na Shule ya Sekondari ya Wasichana Geita ambayo imejengwa katika Manispaa ya Geita huku ikiwa imeanza kutoa huduma za elimu kwa wanafunzi.

Jumla ya Shilingi Bilioni 4.1 zimetolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika shule ya wasichana Geita ikiwemo maabara, vyumba vya madarasa na ofisi, Vyoo vya waliku na wanafunzi, mabweni, nyumba za walimu, Jengo la utawala, Bwalo, Jengo la TEHAMA, na Mashimo ya maji taka.

Pia serikali inaendelea na ujenzi wa shule mpya na ya kisasa ya Amali mkoani Geita ikiwa inajengwa katika Kijiji cha Iboya katika kata na Wilaya ya Mbogwe kwa gharama ya Shilingi Bilioni 1.6

Pia ukamilishaji wa Shule mpya ya Amali ambayo inajengwa ikiwa ni utekelezaji wa sera mpya ya elimu ya mafunzo ya mwaka 2014 toleo la mwaka 2023.

About the author

mzalendoeditor