Featured Kitaifa

TPA MAKAO MAKUU, BANDARI YA TANGA WATEMBELEA WADAU WA KASKAZINI WAPOKEA CHANGAMOTO NA KUHAIDI KUZITATUA

Written by mzalendoeditor

 

NA MWANDISHI WETU, TANGA.

MAAFISA wa Mamlaka ya Usimamizi wa  Bandari Tanzania (TPA) Makao Makuu pamoja na Bandari ya Tanga wamefanya ziara ya kuwatembea wadau wa kanda ya Kaskazini.

Lengo la ziara hiyo ya wadau wa kanda ya Kaskazini inayojumuisha mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Manyara na Arusha ambapo nia ya ziara hiyo ni kuongea na wateja wao ili kuweza kujua changamoto mbalimbali wanazozipata pindi wanapotumia bandari.

Licha ya hivyo pia pamoja na kuwatangazia huduma zinazotarajiwa kutolewa katika Bandari ya Tanga baada ya maboresho makubwa yaliyofanywa.

Hata hivyo wameipongeza Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu kwa maboresho makubwa yanayoendelea katika Bandari Kongwe ya Tanga.

About the author

mzalendoeditor