Featured Kitaifa

BI. OMOLO ATETA NA WATUMISHI WA HAZINA NDOGO MOROGORO

Written by mzalendoeditor


Naibu Katibu Mkuu – Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, akizungumza wakati wa kikao na watumishi wa Ofisi ya Hazina Ndogo mkoani Morogoro, kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina ndogo mkoani Morogoro.

Mkuu wa Hazina Ndogo Mkoa wa Morogoro CPA(T) Robin Kimweri, akizungumza wakati wa kikao na Naibu Katibu Mkuu – Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, kilichowahisha Watumishi wa Ofisi ya Hazina Ndogo mkoani humo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hazina Ndogo mkoani Morogoro.

Msimamizi wa Mali za Serikali Mkoa wa Morogoro, Bw. Khamis Mouktar, akizungumza wakati wa kikao na Naibu Katibu Mkuu – Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, kilichowahisha Watumishi wa Ofisi ya Hazina Ndogo mkoani humo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina Ndogo mkoani Morogoro.

Naibu Katibu Mkuu – Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, akifurahia jambo wakati wa kikao na watumishi wa Ofisi ya Hazina Ndogo mkoani Morogoro, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hazina Ndogo mkoani Morogoro.

Naibu Katibu Mkuu – Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Ofisi ya Hazina Ndogo Morogoro. Kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Idara ya Sera za Ununuzi wa Umma Wizara ya Fedha, Bi. Emma Komba, Mkuu wa Hazina ndogo Mkoa wa Morogoro CPA(T) Robin Kimweri na kulia ni Msimamizi wa Mali za Serikali Mkoa wa Morogoro, Bw. Khamis Mouktar.

Mhasibu wa Ofisi ya Hazina Ndogo, Bw. Benard Mkude, akizungumza wakati wa kikao na Naibu Katibu Mkuu – Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, alipotembelea Ofisi hiyo na kuzungumza na watumishi wa Ofisi ya Hazina ndogo mkoani Morogoro.

Mhakikimali wa Ofisi ya Hazina Ndogo mkoa wa Morogoro, Bi. Halima Majaliwa, akizungumza wakati wa kikao na Naibu Katibu Mkuu – Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, alipotembelea Ofisi hiyo na kuzungumza na watumishi wa Ofisi ya Hazina Ndogo mkoani Morogoro.

Afisa Tehama wa Ofisi ya Hazina Ndogo-Morogoro, Bw. Keith Mshemakweli, akizungumza wakati wa kikao na Naibu Katibu Mkuu – Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, alipotembelea Ofisi hiyo na kuzungumza na watumishi wa Ofisi ya Hazina Ndogo mkoani Morogoro.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Morogoro)

Na. Josephine Majura, WF, Morogoro

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, amewataka Watumishi wa Hazina Ndogo mkoani Morogoro kujiendeleza kimasomo ili kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

Bi. Omolo alisema hayo wakati alipokutana na Watumishi wa Hazina Ndogo, mkoani Morogoro, ambapo pamoja na mambo mengine aliwaahidi Watumishi hao kuwa Wizara itahakikisha inaweka mazingira mazuri ikiwemo kuwapatia mafunzo ya mara kwa mara ili Ofisi hiyo iweze kuwahudumia vyema Wananchi wa Mkoa wa Morogoro na Taifa kwa ujumla.

Kikao hicho cha Naibu Katibu Mkuu, kilihudhuriwa na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Sera za Ununuzi wa Umma, Wizara ya Fedha, Bi. Emma Komba, Mkuu wa Hazina Ndogo Mkoa wa Morogoro CPA(T) Robin Kimweri, Msimamizi wa Mali za Serikali Mkoa wa Morogoro, Bw. Khamis Mouktar, Wahasibu na Wasimamizi wa Mali za Serikali na Watumishi wengine wanaohudumu katika Ofisi ya Hazina Ndogo – Morogoro.

About the author

mzalendoeditor