Featured Kitaifa

MEI MOSI YAFANA NA WAFANYAKAZI TAMISEMI JIJINI DODOMA

Written by mzalendoeditor

  

Asila Twaha, OR – TAMISEMI

Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa wameadhimisha siku ya wafanyakazi Mei Mosi kwa kushiriki maandamano yaliyoanzia katika uwanja wa shule ya Sekondari Centra hadi uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Akiwa ni mgeni rasmi wa sikuku ya Mei Mosi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema, anatambua mchango mkubwa walionao wafanyakazi katika kuchangia uchumi wa nchi na kusema, wafanyakazi hao waendelee kufanya kazi kwa kujituma na uadililifu akiahidi Serikali itaendelea kufanyia kazi maombi yaliyowasilishwa na chama cha wafanyakazi.

Awali akisoma risala Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) Henry Makunda amesema, sababu ya kauli mbiu ya mwaka huu inayosema Mishahara na Maslahi Bora kwa Wafanyakazi ndio kilio chetu Kazi Iendelee” imemaanisha ni muda wa miaka kadhaa tangia wafanyakazi kuongezwa mshahara ikiwa kwa sekta binfasi takribani miaka tisa na seka za umma ni miaka saba amesema, hali hiyo inapelekea kupungua kwa ari ya utendaji kazi kwa wafanyakazi hao.

Aidha, amesema kwa sasa kima cha chini kwa sekta binafsi ni shilingi 40,000 na kwa upande wa umma kima cha chini ni shilingi 300,000 ambapo kima hicho kilitangazwa mwaka 2015.

“Pamoja na nchi yetu kukumbwa na ugonjwa wa UVIKO – 19 na kwa nchi za wenzetu Ukraine na Urusi kuwa na vita ambapo imesababisha kushuka kwa uchumi tunaomba Serikali iangalie namna ya kuongeza mshara kwa wafanyakazi ili kuwezesha kuendelea kumudu maisha” amesema Makunda

Maadhimisho hayo Kitaifa yalifanyika Jijini Dodoma.

About the author

mzalendoeditor