Featured Kitaifa

SERIKALI YAHAMASISHA WADAU KUWEKEZA KATIKA UTALII ENDELEVU

Written by mzalendoeditor

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Khamis Hamza Khamis ametoa wito kwa wadau katika sekta ya utalii kuongeza uwekezaji na juhudi za pamoja katika usimamizi wa utalii katika maeneo yanayolindwa ili kuwa na Utalii endelevu.

Mhe. Khamis ameongeza kuwa kuwekeza katika utalii wa maeneo yaliyolindwa sio tu kunafaida kwa uhifadhi, bali pia unahamasisha maendeleo ya kimkakati ya jamii inayozunguka maeneo hayo.

Akifungua warsha ya kujadili umuhimu wa Uhifadhi, Ukuaji wa Utalii na Ustawi wa Jamii iliyofanyika kwenye hotel ya Mt. Meru jijini Arusha leo tarehe 14.06.2025 amesema ni wakati sasa wadau kujitokeza kwa wingi kuwekeza na kujikita katika usimamizi wa Rasilimali za utalii ili ziweze kutuletea faida kwa jamii na Taifa kwa ujumla.

Pia amesisitiza juu ya umuhimu wa kubadilishana uzoefu utakaosaidia katika kuchunguza fursa zilizopo kwenye Maliasili zitakazoweza kunufaisha jamii kama kichocheo muhimu cha maendeleo.

Amesema bila wanayama hakuna Utalii, bila misitu hakuna utalii hivyo ni vyema tukahamasisha watu kutumia nishati safi ili kuendelea kutunza misitu yetu, kulinda na kuhifadhi wanyama wetu ili utalii uendelee na uingize pato kwa Taifa na jamii ya maeneo husika ipate manufaa.

Akizungumza wakati wa warsha huyo ya Mkurugenzi wa Benki ya Dunia Kanda ya Tanzania Nathan Belete amesema kukuza ushirikiano kati ya wadau ni njia bora ya kusaidia juhudi za uhifadhi.

“Utafiti umeonesha kuwa utalii katika maeneo yanayolindwa una faida kubwa, unatoa ajira, na unaingiza Taifa pato kubwa ambalo hurudishwa kwa jamii kwa kuwekezwa katika miradi ya maendeleo’

Alibainisha kuwa, katika baadhi ya nchi, kila dola moja iliyowekezwa katika maeneo yanayolindwa huzalisha hadi dola 28 ambapo ni faidi kwa jamii na Taifa lwa ujumla.

Naye Mkurugenzi wa Utekelezaji wa Kanda kutoka Benki ya Dunia Anna Wellenstein amesisitiza umuhimu wa ushirikiano na mafunzo

“Warsha hii imetujengea uwezo kwamba rasilimali asilia si muhimu tu kwa bioanuai ila pia ni injini yenye nguvu katika ukuaji wa uchumi na maendeleo ya jamii,” alisema.

Amesema mkutano huu wa siku mbili umtengeneza jukwaa lililowezesha washiriki kujifunza kutoka kwa kila mmoja kati ya nchi na nchi, Taasisi kwa Taasisi, Sekta binafsi pamoja na wadau wa utalii.

Warsha hii ya siku mbili imehudhuriwa na wataalamu wa kitaifa na kimataifa zaidi ya 100 kutoka katika Taasisi za Serikali, mashirika ya kiraia, sekta binafsi, na washirika wa maendeleo kujadili mambo muhimu ya kuhifadhi, utalii na maendeleo ya jamii.     

About the author

mzalendoeditor