Baada kuitumikia Barcelona kwa karibu miongo miwili Lionel Messi alijiunga na PSG msimu uliopita baada ya klabu hiyo kushindwa kumsainisha nyongeza ya mkataba mpya kutokana na tatizo la uchumi.
Barça ilipaswa kuuza na kupunguza mishahara ya baadhi ya wachezaji klabuni hapo huku Jordi Alba na Sergio Busquets wakikubali kukatwa mishahara.
Kwa mujibu wa jarida la El Pais, Gerald Pique alimwambia Rais wa Barça Joan Laporta kuondoka kwa Messi ndio Suluhu ya kuinusuru klabu hiyo na rungu la FFP.
Inaelezwa hata uamuzi wa Pique kukubali kukatwa mshahara ulikuja baada ya Messi kuondoka wakati angefanya uamuzi huo mapema Messi angebaki.
Hali hiyo imepelekea kuvunjika kwa urafiki wa muda mrefu wa wawili hao huku Messi akihisi kusalitiwa na rafiki yake huyo.
Mnamo Jan 24 wakati wa mapumziko ya mechi za kimataifa Messi aliwaalika Busquets na Jordi Alba pekee katika tafrija fupi ya Jioni akikataa kumwalika Pique.