WAZIRI wa Afya Mhe.Jenista Mhagama,akiwalisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2025 leo Juni 2,2025 bungeni Dodoma.
Na.Alex Sonna_DODOMA
KATIKA kipindi cha Julai 2024 hadi Machi 2025, takribani watu milioni 20 walipatiwa elimu kuhusu magonjwa yasiyoambukiza na afua za kuzuia na kudhibiti magonjwa hayo kupitia njia mbalimbali ikiwemo usambazaji wa nakala ngumu 15,050 za kitabu cha mtindo bora wa Maisha.
Hayo yameelezwa leo Juni 2,2025 na Waziri wa Afya,Jenista Mhagama wakati akiwaslisha bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2026.
Waziri Jenista amesema katika kukabiliana na tatizo la magonjwa yasiyoambukiza, Serikali imeimarisha afua za udhibiti katika ngazi zote ikijumuisha udhibiti katika ngazi ya jamii, mashuleni na mahali pa kazi.
Amesema katika kipindi cha Julai 2024 hadi Machi 2025, takribani watu milioni 20 walipatiwa elimu kuhusu magonjwa yasiyoambukiza na afua za kuzuia na kudhibiti magonjwa hayo kupitia njia mbalimbali ikiwemo usambazaji wa nakala ngumu 15,050 za kitabu cha mtindo bora wa Maisha.
Pia kuelimisha kuhusu ugonjwa wa kisukari, udhibiti wa pombe na tumbaku pamoja na nakala laini za ujumbe mfupi na kurusha video fupi zaidi ya 10,000 kupitia mitandao ya kijamii.