Featured Kitaifa

AJALI YAUA POLISI NA MAHABUSU 

Written by mzalendoeditor

Watu wanne wakiwemo askari polisi wawili na mahabusu wawili – waliokuwa wakituhumiwa kwa makosa ya kujihusisha na vitendo vya kigaidi pamoja na mauaji, wamepoteza maisha kwa ajali ya gari iliyotokea jana Jumatano jioni Aprili 27, 2022 katika Kijiji cha Ibanda barabara ya Geita-Sengerema.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe amesema chanzo cha ajali hiyo ni gari la polisi aina ya Toyota Landcruise yenye namba za usajili PT 3798 lililokuwa likitokea mkoani Mwanza, kukata ‘sterling rod’ na kuhama kutoka upande wake na kwenda upande mwingine na kugongana na Lori aina ya Scania lenye tela namba. T.865 mali ya kampuni ya Nyanza Botling.

Ajali hiyo pia imejeruhi watu wanne na wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Geita huku miili ya askari hao wawili ikihifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza.

About the author

mzalendoeditor