Timu ya ufatiliaji wa shughuli za afya ikiongozwa na Mkurugenzi wa Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii OR-TAMISEMI, Dkt. Ntuli Kapologwe ( aliyevaa suti ya kijivu)akuzungumza na wananchi wa Halmashauri ya Ngara
Mkurugenzi wa Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii Dkt. Ntuli Kapologwe akikagua ujenzi wa Jengo la mama na mtoto katika Kituo cha Afya Mgoma kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngaratarehe
Ujenzi wa jengo la wodi ya mama na mtoto na jengo la upasuaji katika kituo cha afya Mgoma kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya Ngara.
………………………………………………….
OR-TAMISEMI
Timu ya ufatiliaji wa shughuli za afya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imeridhishwa na ujenzi wa miundombinu ya kutolea huduma za afya katika vituo vya afya unaotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara.
Timu hiyo imeipongeza Halmashauri ya Ngara kwa usimamizi mzuri na kuitaka Halmashauri hiyo kufanya ukarabati mdogomdogo kwenye maeneo ambayo yamebainishwa kuwa na mapungufu.
Wito huo umetolewa 27 Aprili 2022 katika ziara ya usimamizi shirikishi uliofanywa na timu hiyo kufatilia utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu ya kutolea huduma za afya katika Halmashauri hiyo.
Aidha timu hiyo imeitaka Kamati tendaji ya usimamizi wa shughuli za afya katika Halmashauri hiyo kufanya ukaguzi na kuimarisha usimamizi wa dawa na vifaa tiba katika vituo vya afya ili kuepusha upotevu.
Kwa upande mwingine timu hiyo imewataka madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara kushirikiana na Serikali katika kusimamia ujenzi wa miundombinu ya kutolea huduma za afya ili kuimarisha ulinzi shirikishi lakini pia kurahisisha utekelezaji utakaopelekea ujenzi huo ukamilike kwa wakati na kwa viwango vinavyohitajika.
Katika Halmashauri hiyo timu ya ufatiliaji wa shughuli za afya ilitembelea na kukagua ujenzi wa miundombinu katika Hospitali ya Wilaya ya Ngara,ujenzi wa kituo cha afya Mgoma pamoja na kituo cha afya Lusumo