Featured Kitaifa

TANZANIA KUNG’ARA KATIKA SIKU YA KITAIFA  EXPO 2025 OSAKA JAPAN

Written by mzalendoeditor

 

Tanzania ina malengo madhubuti katika ushiriki wake kwenye Maonesho ya Kibiashara ya Kidunia Expo 2025 Osaka Japan kwa kutangaza fursa za biashara, kuvutia uwekezaji na kuonesha urithi wake katika tamaduni na desturi katika maonesho hayo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt Selemani Jaffo wakati akizungumzia umuhimu wa Siku ya Tanzania yaani (Tanzania Day) itakayofanyika tarehe 25 /05/2025 na
Kongamano la Biashara, Uwekezaji na Utalii litakalofanyika
tarehe 26 Mei 2025 zinazolenga
kunadi fursa za uwekezaji zilizopo nchini kwa lengo la kuvutia wawezekaji katika sekta mbalimbali ikiwemo maliasili, utalii, kilimo, viwanda na biashara na kutilia mkazo kuhusu fursa kubwa iliyopo katika uwekezaji katika joto ardhi.

Aidha Dkt. Jafo amewakaribisha wadau na wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali kushirikiana na Tanzania katika uwekezaji kwenye maeneo mbalimbali.

About the author

mzalendoeditor