Featured Kitaifa

MAADHIMISHO SIKU YA MALARIA DUNIANI YAFANYIKA TARIME, SERIKALI IKISISITIZA WANANCHI KUTOTUMIA DAWA BILA KUPIMWA

Written by mzalendoeditor

Madaktari kutoka hospitali ya wilaya ya Tarime wakihudumia watoto wakati wa maadhimisho ya Siku ya Malaria yaliyofanyika katika viwanja vya Sekondari ya Igwe wilayani humo chini ya udhamini wa Barrick North Mara.
***
 
Serikali wilayani Tarime, imewataka wananchi kuzingatia ushauri wa kitaalamu wa kupambana na ugonjwa hatari wa Malaria ili kupunguza maambukizi na vifo.
 
Wito huo ulitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Michael Mtenjele, kwenye Maadhimisho ya Siku ya Malaria wilayani Tarime ambayo yalifanyika katika viwanja vya shule ya sekondari ya Igwe chini ya udhamini wa kampuni ya madini ya Barrick kupitia mgodi wake wa North Mara.
 
Mtenjele, alisema wananchi wanapojisikia hali zao sio nzuri ni muhimu kwenda kupima afya zao kwenye vituo vya afya badala ya kununua dawa na kuzitumia bila kupima,pia alihimiza wananchi kuzingatia matumizi ya vyandarua kwa usahihi sambamba na kusafisha mazingira kwenye maeneo yao ili kuondoa mazalio ya mbu.
 
Kwa upande wake, Matibu wa Malaria wilayani humo, ,Dk. Amos Manya,alieleza kuwa ugonjwa wa Malaria unaambukizwa na mbu jike aina ya Anofelesi aliyebeba vimelea vya Malaria toka kwa mtu mwenye vimelea na kwenda kwa mtu asiye na vimelea mara pale anapomuuma mtu huyo na kwamba maambukizi hayo huleta madhara makubwa na vifo katika jamii
 
Amezitaja dalili za ugonjwa wa malaria kuwa ni homa, maumivu ya kichwa, kutapika, kuharisha, mwili kuchoka/kuregea na kukosa nguvu na kukosa hamu ya kula.
 
Amewataka wananchi kuwahi mapema kwenye vituo vya afya pindi waonapo dalili za malaria ili kupata matibabu sahihi na kumaliza matibabu yote.
Maadhimisho hayo yaliambatana na Wananchi waliohudhuria kupima afya zao, pia zilikuwepo huduma za kiafya kwa watoto na akina mama Wajawazito.
Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Michael Mtenjele, akihutubia wageni waalikwa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Malaria yaliyofanyika katika viwanja vya Sekondari ya Igwe,wilayani humo chini ya udhamini wa Barrick North Mara.
 

 

Mratibu wa Malaria wa Wilaya ya Tarime Dk. Amos Manya, akihutubia wageni waalikwa wakati wa maadhimisho hayo

 

Wanafunzi kutoka shule mbalimbali wilayani humo walihudhuria maadhimisho hayo.
Wasanii kutoka vikundi mbalimbali walikuwepo kwa ajlli ya kupamba maonyesho hayo

About the author

mzalendoeditor