WAZIRI wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo ,akizungumza na Waandishi wa Habari leo Mei 15,2025 jijini Dodoma kuhusu Mafanikio ya Wizara hiyo katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Na.Alex Sonna_DODOMA
Waziri wa Viwanda na Biashara,Selemani Jafo amelitaka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kutoa Elimu kwa watanzania kuhusu madhara ya unywaji wa pombe uliopitiliza kwani unapunguza nguvu kazi ya Taifa.
Jafo ametoa agizo hilo,leo Mei 15,2025 wakati akieleza mafanikio ya miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita mbele ya Waandishi wa Habari.
Waziri Jafo amesema kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda,Biashara,kilimo na mifugo ilisema bado Kuna changamoto ya ulevi uliopitiliza katika jamii Hali ambayo imekuwa ikipoteza nguvu kazi.
“Sasa nazielekeza taasisi zangu kutoa elimu kwa umma kuhusu unywaji wa pombe.Niwaombe watanzania tubadilishe unywaji ni hatari sana,utahatibu Taifa,”amesema Waziri Jafo.