WAZIRI wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo ,akizungumza na Waandishi wa Habari leo Mei 15,2025 jijini Dodoma kuhusu Mafanikio ya Wizara hiyo katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Na.Alex Sonna_DODOMA
WAZIRI wa Viwanda na Biashara,Selmani Jafo amesema Takwimu zinaonesha kwa sasa kuna Viwanda zaidi ya 80,000 ambavyo vimetoa ajira kwa zaidi ya watanzania milioni 5.
Kauli hiyo ameitoa leo Mei 15,2025 Jijini Dodoma,wakati akieleza mafanikio ya miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita.
Waziri Jafo amesema Takwimu zinaonesha kwa sasa kuna Viwanda 80,000 ambavyo vingi ni vidogo ambavyo vimetoa ajira zaidi ya milioni tano.
Aidha,amesema Serikali inakuja na Mpango wa sensa ya Viwanda ambao utaanzia Mkoani Mwanza na Shinyanga lengo likiwa ni kuhakikisha inapata idadi ya Viwanda,vikubwa vya kati na vidogo
Vilevile,Waziri Jafo amemshukuru Rais Samia kwa kufungua fursa za Biashara na uwepo wa Viwanda vingi nchini.