Featured Kitaifa

TAKWIMU ZA ELIMU KUWA KATIKA MFUMO MMOJA

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Adolf Mkenda,akiwasilisha bungeni Jijini Dodoma makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2025-2026.

Na Alex Sonna,Dodoma

WIZARA ya Elimu,Sayansi na Teknolojia inajivunia kuunganisha  mifumo ya takwimu za elimu na kuwa na mfumo mmoja wa sekta ya elimu.
Hayo yameelezwa leo Mei 12,2025 bungeni na Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Adolf Mkenda wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2026.
Waziri Mkenda amesema takwimu za elimu ni nyenzo muhimu katika kuboresha ufundishaji na ujifunzaji, kufanya tafiti na kutoa maamuzi mbalimbali.
“Kwa kutambua umuhimu huo,
Serikali imeunganisha mifumo ya takwimu za
elimu na kuwa na mfumo mmoja wa sekta ya elimu,”amesema Waziri Mkenda
Aidha,Wizara  imeendelea na ujenzi wa Mfumo wa Takwimu wa Sekta ya Elimu utakaowezesha
upatikanaji wa takwimu zote za sekta kupitia
mfumo huo.
 Aidha, mfumo huo utakuwa na uwezo
wa kupokea takwimu mbalimbali zinazohusiana na
elimu kutoka katika mifumo mingine ya Serikali ikiwemo NIDA, RITA, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Idara ya Uhamiaji na OR–TAMISEMI.

About the author

mzalendoeditor