Featured Kitaifa

MHE.KATANI AKUNWA NA UWEZO WA AWESO ADAI KATIKA MAWAZIRI WATATU BORA YUMO

Written by mzalendoeditor
MBUNGE  wa Tandahimba (CCM),Mhe. Katani Ahmed Katani, akichangia mjadala wa makadirio ya  mapato na matumizi ya Wizara ya Maji kwa mwaka 2025-2026  leo Mei 9,2025 bungeni jijini Dodoma.
…..
 MBUNGE  wa Tandahimba (CCM),Mhe. Katani Ahmed Katani,amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kama Mbunge wa Pangani,Juma Aweso atarudi tena bungeni katika uchaguzi ujao basi  amrejeshe katika nafasi yake ya uwaziri wa Maji ili aweze kukamilisha yale mambo mazuri yaliyobaki.
Mhe.Katani ameyasema hayo leo Mei 9,2025 bungeni jijini Dodoma wakati akichangia mjadala wa makadirio ya  mapato na matumizi ya Wizara ya Maji kwa mwaka 2025-2026.
Mbunge huyo amesema kama angepewa nafasi ya kuchagua mawaziri watatu bora basi asingeacha kumchagua Aweso kwani amefanya kazi kubwa.
Kutokana na hali hiyo amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kama Mbunge huyo atachaguliwa na wananchi wa Jimbo la Pangani basi amrejeshe katika nafasi yake ya uwaziri wa maji.
“Sisi watu wa  Mtwara hususani  Newal ana Tandahimba ni watu ambao tumepata shida ya  maji kwa muda mrefu na tumekuwa na mradi wa Makonde  tangu tumepata uhuru haikuwahi kutengewa fedha lakini wakandarasi wapewa  bilioni 84.7 katika mambo ambayo tunafikiria yanayofanywa na Rais Sania hatuna sababu 2025 kupoteza kura,tutampa yeye,”amesema Mhe.Katani

About the author

mzalendoeditor