Na Amiri Kilagalila,Njombe
Mpiga debe mmoja wa eneo la Makambako mkoani Njombe amefariki dunia kwa kukanyagwa na gari katika kichwa chake kutokana na kuanguka wakati akifukuzia basi linalofanya safari zake kutoka Mbeya kwenda mkoani Mwanza ili aweze kupata posho yake ya kupakia abiria.
Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issah amethibitisha hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
“Mpiga debe alikuwa amefuata fedha yake kwa ajili ya abiria aliokuwa amewapakia na kwa bahati mbaya ule malango wakati unajifunga aliweza kusukumwa na akadondokea kwenye uvungu na tairi za nyuma za gari ziliweza kumpitia”alisema Kamanda Issah
Ametoa wito kwa wafanyakazi wa maeneo ya stendi kuwa makini na kuangalia usalama wao wakati wa kufanya kazi zao.