Featured Michezo

WAZIRI MCHENGERWA ATETA NA WAWEKEZAJI WA MIUNDOMBINU YA MICHEZO

Written by mzalendoeditor

   

Na. John Mapepele

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amekutana na kufanya mazungumzo na baadhi ya wawekezaji wa kujenga miundombinu ya michezo ambao wameonyesha nia ya kujenga miundombinu ya kisasa ya michezo hapa nchini.

Mhe. Mchengerwa ameambatana na Watendaji kadhaa wa Wizara yake kwenye Sekta ya Michezo wakiongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo nchini, Yusufu Omary Singo wamekutana na wawekezaji hao na kufanya mazungumzo leo Aprili 22, 2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mhe, Mchengerwa amekutana na wawekezaji hao kufuatia dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kutaka kuinua kiwango cha michezo nchini kufikia ngazi ya kimataifa kwakuwa na mkakati wa kuwekeza katika ujenzi wa miundombinu ya kisasa ya michezo kote nchini.

Kwa sasa Serikali inakusudia kujenga miundombi ya kisasa ikiwa ni pamoja na viwanja vya michezo, Sanaa na arena pia kuwa na miundombinu ya kisasa ya michezo kwa shule mbili kila mkoa.

About the author

mzalendoeditor