Featured Kitaifa

TUME YAWATAKA WAENDESHA BVR DAR KUFUATA SHARIA, KUTUNZA VIFAA

Written by mzalendo
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele (katikati) akizungumza  na washiriki wa mafunzo ya siku mbili ya Waandikishaji Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Bayometriki kwa Jimbo la Ukonga Halmashauri ya Jiji la Daes Salaam alipotembelea mafunzo hayo Machi 14,2025. (Pichja na INEC).  

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele (katikati) akizungumza  na washiriki wa mafunzo ya siku mbili ya Waandikishaji Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Bayometriki kwa Jimbo la Ukonga Halmashauri ya Jiji la Daes Salaam alipotembelea mafunzo hayo Machi 14,2025. Kulia ni Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Dar es Salaam, Ndg. Gerald Sondo na Kushoto ni Afisa Mwandikishaji wa Jiji la Dar es Salaam, Adv. Faraja Nakua. (Pichja na INEC). 

 

Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama Kuu, Asina Omari, akizungumza wakati alipotembelea mafunzo ya siku mbili kwa watendaji hao, katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke. ambapo aliwataka Waandikishaji Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Bayometriki, wametakiwa kutumia kauli nzuri kwa wananchi, wakati wanatekeleza majukumu yao kwenye vituo vya kuandikisha wapiga kura.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya siku mbili ya Waandikishaji Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Bayometriki kwa Jimbo la Ukonga Halmashauri ya Jiji la Daes Salaam wakiwa katika mafunzo hayo. 

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya siku mbili ya Waandikishaji Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Bayometriki kwa Jimbo la Ukonga Halmashauri ya Jiji la Daes Salaam wakiwa katika mafunzo hayo. (Picha na INEC). 

*******************

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC)
imewataka Waandikishaji Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Bayometriki (BVR)
kutekeleza majukumu yao vituoni kwa kufuata sharia, Kanuni na Taratibu za Tume
pamoja na umakini katika utunzaji vifaa.


 Hayo yamesemwa leo Machi 14, 2025 na
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs
Mwambegele wakati alipotembelea na kuzungumza na washiriki wa mafunzo ya siku
mbili ya Waandikishaji Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Bayometriki kwa Jimbo
la Ukonga Halmashauri ya Jiji la Daes Salaam.

“Katika kufanya kazi ambayo kwayo
mnafundishwa hivi leo, mkafanye kwa kufuata Sheria, Kanuni na taratibu, vyote
hivyo mtafundishwa lakini pale ambapo utaona umekwama usisite kuwasiliana na
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ili usikwamishe zoezi,” alisema Jaji wa Rufani
Mwambegele.

Aidha, Jaji Mwambegele aliwataka washiriki
ambao ndio wanakwenda kutekeleza jukumu la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la
Wapiga Kura Mkoa wa Dar es Salaam kuhakikisha wanatunza vifaa watakavyo
kabidhiwa.

Jaji Mwambegele alisema vifaa hivyo
vimetumika nchi nzima kwa mizunguko 12 ambayo Tume iliipanga na sasa ipo
mzunguko wa 13 unaotaraji kutekelezwa Mkoani Dar es Salaam kuanzia Machi 17
hadi 23, 2025 kwa kutumia vifaa hivyohivyo na vinapaswa kutunzwa kwani
vitatumika pia katika awamu ya pili ya zoezi la uboreshaji nchi nzima.

“Vifaa hivi isingekuwa kutunza vyema
msingekuwa hapa leo, vifaa hivi vimenunuliwa na kodi za wananchi kwa bei ya juu
sana hivyo nawaomba mvitunze vifaa hivi kwanza wakati huu wa mafunzo lakini pili
wakati wa zoezi lenyewe,” alisema Jaji Mwambegele.
 
Akitembelea mafunzo kama hayo katika
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Mkoani Dar es Salaam, Mjumbe wa Tume Mhe.
Jaji Asina Omari amewataka Waandikishaji Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya
Bayometriki, kuzingatia mafunzo ya nadharia pamoja na vitendo ili wakaweze
kufanya kazi hiyo kwa ufanisi.

Mapema akifungua mafunzo hayo baada ya
kuwaapisha washiriki hao kiapo cha kujitoa unachama na kile cha kutunza siri,
Afisa Mwandikishaji wa Jiji la Dar es Salaam, Adv. Faraja Nakua aliwataka
washiriki hao kufanya kazi kwa weledi na kuwa na lugha nzuri kwa wananchi.

“Mtakapokua vituoni zingatieni weledi wa kazi,
nidhamu, kujituma na bidi ya kazi na lugha nzuri kwa wateja wetu, wateja wetu
ni Wapiga Kura watakao jitokeza kwaajili ya kuboresha au kujiandikisha au kutoa
taarifa za kufutwa kwa mpiga Kura aliyepoteza sifa ya kuwepo kwenye Daftari,”alisema
Nakua.

Mafunzo hayo ya siku mbili yaliyoanza leo
Machi 14 na kutaraji kutamatika Machi 15 mwaka huu ni maandalizi kuelekea zoezi
la Uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura Mkoa wa Dar es salaam kuanzia
Machi 17 hadi 23,2025.
 
Waandikishaji Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Bayometriki kutoka Jimbo la Ukonga Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaa wakila kiapo cha kujitoa uanachama na kile cha kutunza siri leo Machi 14,2025 kabla ya kuanza kwa mafunzo ya siku mbili kuhusu Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. (Picha na INEC). 
Afisa Mwandikishaji wa Jiji la Dar es Salaam, Adv. Faraja Nakua  akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo akiwa na maafisa kutoka Tume, Bi. Fina Kidunda na Nicolaus Natay. 

Afisa kutoka INEC, Bi Fina Kidunda akifafanua jambo wakati wa mafunzo hayo. 

Washiriki kutoka Temeke wakiwa katika mafunzo hayo.

About the author

mzalendo