Uncategorized

DK.CHAULA AWATAKA WATUMISHI KUTIMIZA MAJUKUMU YAO

Written by mzalendoeditor

Na WMJJWM, Lushoto

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula ametoa wito kwa watumishi Wilayani Lushoto mkoani Tanga kutimiza majukumu yao kwa ufanisi kulingana na taaluma zao badala ya kukaa kusubiri maelekezo ya viongozi.

Ameyasema hayo Wilayani hapa wakati wa ziara ya kikazi yenye lengo la kukagua utekelezaji wa shughuli zinazozimamiwa na Wizara katika ngazi ya Mkoa na Halmashauri.

Dkt. Chaula amesema watumishi Wana wajibu wa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria na Miongozo iliyopo na sio kusubiri kusukumwa kwa kusubiri maagizo ya Viongozi wa ngazi za juu.

“Maelekezo tayari yamo kwenye sera, sheria na miongozo mbalimbali, tufanye kazi Kwa matokeo, lazima tubadilishe fikra zetu” amesema Dkt. Chaula.

Akiwa wilayani hapa Dkt. Chaula ametembelea na kukagua ujenzi wa madarasa mawili katika chuo cha Maendeleo ya Jamii Mabughai yaliyojengwa na wanafunzi kutokana na mafunzo wanayopata pamoja na kuzungumza na watumishi wa chuo hicho.

About the author

mzalendoeditor