Featured Kitaifa

WANAWAKE TUME YA KUREKEBISHA SHERIA TANZANIA WATOA MSAADA KITUO CHA WASIOONA WATU WAZIMA BUIGIRI

Written by mzalendoeditor
KUELEKEA Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani, Wanawake kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania wametembelea Kituo cha Wasioona Watu Wazima kilichopo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma na kutoa msaada wa mahitaji mbalimbali.
Akizungumza mara baada ya kufika katika kituo hicho,Naibu katibu Mkuu Tume ya kurekebisha sheria Bi. Zainabu Chanz amesema
Bi.Zainabu amesema kuwa  katika kipindi hiki cha kuelekea maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani, wanawake wa wanakumbushwa kutimiza wajibu wao kwa jamii kama wazazi kwa ustawi wa jamii yetu.
“Wao kama wakinamama wameona ni vyema kuadhimisha siku hiyo kwa kutoa misaada mbalimbali kwa  wahitaji hao ikiwemo Mchele Kg100, Maharage Kg100, Mipira ya kumwagilia maji 2, Unga sembe Kg100, Chumvi Pisi 80, Mafuta ya kula Lita 40, Sabuni za Unga mifuko 2 sawa na pisi 60″amesema
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kituo hicho Mzee Yaledi Chereso amesema kuwa kituo hicho wanaishi kwa kujitegemea wenyewe na misaada kutoka wa wadau mbalimbali hivyo kwa ujio wao umeleta matumaini ma  faraja katika kituo hivyo
Aidha Mzee Chereso ametoa ombi kwa tume hiyo kuwapatia  elimu ya sheria kutoka kwa wataalamu hao ili kujua haki zao za msingi kama walemavu kwani kwakufanya hivyo kutaleta mshikamano na  kupinga ukatiki wa kijinsi
Naye   Mmoja wa wanaoishi katika kituo hicho Vumilia Sara Mgandu,ameeleza kuwa ingawa anasumbuliwa na ulemavu wa macho lakini anajishughulisha na utengenezaji wa sabuni za maji, kuku na ndizi (Ujasiriamali) hivyo ameshukuru kwa misaada hiyo ikiwemo kumuungisha bidhaa zake.

About the author

mzalendoeditor