Featured Kitaifa

WASAIDIZI WA SHERIA 300 WAPEWA MAFUNZO MAALUM KUHUSU MSAADA WA KISHERIA NCHINI

Written by mzalendoeditor

 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Franklin Rwezimula,akizungumza  wakati akifungua mafunzo maalum kwa wasaidizi wa kisheria leo Februari 26,2025 jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Franklin Rwezimula,akizungumza  wakati akifungua mafunzo maalum kwa wasaidizi wa kisheria leo Februari 26,2025 jijini Dodoma.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Legal Services Facility (LSF),Bw. Amani Manyelezi,akizungumza  wakati wa mafunzo maalumkwa wasaidizi wa kisheria kuhusu msaada wa kisheria leo Februari 26,2025 jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Franklin Rwezimula (hayupo pichani),akizungumza  wakati akifungua mafunzo maalum kwa wasaidizi wa kisheria leo Februari 26,2025 jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt.Franklin Rwezimula,akipokea zawadi kutoka kwa Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Legal Services Facility (LSF),Bw. Amani Manyelezi,mara baada ya kufungua mafunzo maalum kwa wasaidizi wa kisheria leo Februari 26,2025 jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Franklin Rwezimula,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua mafunzo maalum kwa wasaidizi wa kisheria leo Februari 26,2025 jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Franklin Rwezimula,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua mafunzo maalum kwa wasaidizi wa kisheria leo Februari 26,2025 jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Franklin Rwezimula,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua mafunzo maalum kwa wasaidizi wa kisheria leo Februari 26,2025 jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA
JUMLA ya wasaidizi wa kisheria 300 wanatarajiwa kupatiwa mafunzo maalum kuhusu sheria zilizopo, kanuni, miongozo, na sera zinazohusiana na utoaji wa msaada wa kisheria nchini.
Akizungumza leo Februari 26,2025 jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo hayo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Franklin Rwezimula,amesema  serikali inaendelea kuboresha mifumo ya msaada wa kisheria kwa kuanzisha Madawati ya Msaada wa Kisheria katika halmashauri zote nchini.
Dkt. Rwezimula ameeleza lengo la mafunzo hayo nikuwajengea uwezo wasaidizi hao, maarufu kama paralegals, ili waweze kuendelea kutoa elimu na huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi bila malipo, hususan katika maeneo ya pembezoni.
“Lengo la serikali ni kuhakikisha kila kata inakuwa na msaidizi wa kisheria. Hadi sasa idadi yao bado ni ndogo, lakini jitihada zinaendelea ili kufanikisha azma hii na mafunzo hayo yatafanyika kwa awamu nne, ambapo awamu ya kwanza inahusisha washiriki 42 kutoka mikoa ya Arusha, Dodoma, Singida, Manyara, na Tanga. Mafunzo hayo yatadumu kwa siku 15.,” amesema  Dkt. Rwezimula.
Aidha ametoa wito kwa washiriki wa mafunzo hayo kutumia fursa hiyo kuimarisha ujuzi wao na kutoa huduma kwa wananchi kwa moyo wa kujitolea, hasa kwa makundi yenye uhitaji mkubwa wa msaada wa kisheria.
 “Nataka taasisi kushirikiana na Wizara katika kuwezesha wasaidizi wa kisheria kwa kuwajengea uwezo katika masuala mbalimbali ya kisheria. Pia, aliwataka kuandaa na kufanya Kongamano la Mwaka la Wasaidizi wa Kisheria, ambalo litakuwa fursa ya kujadiliana kuhusu changamoto na fursa wanazokutana nazo katika utoaji wa huduma za msaada wa kisheria nchini.”amesema
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Legal Services Facility (LSF),Bw. Amani Manyelezi, amesema mfuko huo umekuwa ukiunga mkono msaada wa kisheria kwa zaidi ya miaka 12 kwa kushirikiana na mashirika 184 na wasaidizi wa kisheria zaidi ya 3,000 nchini.
“Tunalenga kuweka mazingira wezeshi kwa wasaidizi wa kisheria kwa kushirikiana na Wizara ya Katiba na Sheria, huku tukizingatia usawa wa kijinsia na kupambana na ukatili wa kijinsia, hasa dhidi ya wanawake na watoto,” amesema Bw.Manyelezi.
Hata hivyo amefafanua kuwa kila mwaka wasaidizi wa kisheria wanawafikia zaidi ya wananchi milioni 6, wengi wao wakiwa wa maeneo ya vijijini ambako huduma za msaada wa kisheria ni adimu.
Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 59 ya kesi zinazowasilishwa kwa wasaidizi wa kisheria hutolewa na wanawake, huku asilimia 41 zikihusisha wanaume. Kesi nyingi zinahusiana na masuala ya ndoa na mgawanyo wa mali.
Naye Msajili wa Watoa Huduma za Msaada wa Kisheria, Laurent Burilo-Mwakilfehi, amesema licha ya kuwepo kwa wasaidizi wa kisheria 2,205 waliosajiliwa, bado kuna upungufu mkubwa wa wataalamu hao, hususan vijijini.
“Huduma ya msaada wa kisheria ni bure, hivyo tunawasihi wasaidizi wa kisheria kufanya kazi kwa uzalendo na moyo wa kujitoa. Hii ni kazi ya kiuchungaji, malipo yake ni kuona haki inatendeka kwa jamii,” amesema  Burilo-Mwakilfehi.
Mafunzo hayo yatadumu kwa muda wa miezi miwili na nusu, ikiwa ni sehemu ya programu ya miezi mitatu ya mafunzo kwa vitendo, kabla ya wahitimu kupatiwa vyeti rasmi na kusajiliwa kama wasaidizi wa kisheria.

About the author

mzalendoeditor