RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Wafanyabiashara Mama lishe katika Soko la Jumbi Wilaya ya Magharibi “B” Unguja wakati wa ziara yake kutembelea Soko hilo kuangalia mwenendo wa biashara na upatikanaji wa bidhaa, iliyofanyika leo 24-2-2025.(Picha na Ikulu)
………..
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameeleza kuridhishwa na upatikanaji wa Bidhaa za Vyakula na kuwataka Wafanyabiashara Kutopandisha Bei wakati Ramadhani itakapoanza.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo alipotembelea Masoko ya Jumbi , Mwanakwerekwe na Darajani kuangalia Mwenendo wa Biashara na Upatikanaji wa Bidhaa za Vyakula kuelekea Mwezi Wa Ramadhani.
Aidha Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa Serikali inajipanga kwa ajili ya Ujenzi wa Masoko mengine maeneo mbalimbali ili kila Mfanyabiashara afanye biashara kwenye mazingira rasmi .
Kuhusu Suala la Usafi wa Masoko ameuagiza Uongozi wa Masoko hayo kutafuta njia Bora zaidi ya Uhifadhi wa Bidhaa za Wafanyabiashara ili Masoko kuwa safi wakati Wote.
Amezielekeza Taasisi zinazosimamia Masoko hayo kuhakikisha Upatikanaji wa Huduma ya Maji na Vipooza hewa katika Masoko yote pamoja na kuimarisha Usafi.
Ziara hiyo ya Rais Dkt, Mwinyi ni ya Kwanza tangu kufunguliwa kwa Masoko Mapya ya Jumbi , Mwanakwerekwe na Ukarabati Mkubwa wa Soko la Darajani.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika ziara yake kutembelea Soko la Jumbi Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 24-2-2025, kuangalia mwenendo wa biashara na upatikanaji wa bidhaa katika soko hilo (kulia kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za SMZ Mhe. Masoud Ali Mohamed.(Picha na Ikulu).
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrisa Kitwana Mustafa, alipowasili katika viwanja vya Soko la Jumbi Wilaya ya Magharibi “B” Unguja, akiwa katika ziara yake kutembelea soko la jumbi kuangalia mwenendo wa biashara na upatikanaji wa bidhaa katika masoko ya Jumbi,Mwanakwerekwe na Darajani, ziara hiyo iliyofanyika leo 24-2-2025.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, akimsikiliza Mfanyabiashara wa mbogamboga katika Soko la Jumbi Wilaya ya Magharibi “B” Unguja, wakati wa ziara yake kutembelea Soko hilo kuangalia mwenendo wa biashara na upatikanaji wa bidhaa mbalimbali katika Soko hilo, ziara hiyo iliyofanyika leo 24-2-2025, na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrisa Kitwana Mustafa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, akimsikiliza Mfanyabiashara wa mbogamboga katika Soko la Jumbi Wilaya ya Magharibi “B” Unguja, wakati wa ziara yake kutembelea Soko hilo kuangalia mwenendo wa biashara na upatikanaji wa bidhaa mbalimbali katika Soko hilo, ziara hiyo iliyofanyika leo 24-2-2025, na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrisa Kitwana Mustafa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said.(Picha na Ikulu).
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, akiuliza swali kwa Mfanyabiashara wa mchele Stella Job, katika Soko la Jumbi Wilaya ya Magharibi “B”Unguja, wakati wa ziara yake kutembelea masoko ya Mkoa wa Mjini Magharibi leo 24-2-2025, Soko la Jumbi,Mwanakwerekwe na Darajani. (Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, akiangalia bidhaa ya mchele wakati wa ziara yake katika Soko la Jumbi Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 24-2-2025, kuangalia mwenendo wa biashara na upatikanaji wa bidhaa katika soko hilo.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Wafanyabiashara Mama lishe katika Soko la Jumbi Wilaya ya Magharibi “B” Unguja wakati wa ziara yake kutembelea Soko hilo kuangalia mwenendo wa biashara na upatikanaji wa bidhaa, iliyofanyika leo 24-2-2025.(Picha na Ikulu)