Featured Kitaifa

WANANCHI MANISPAA YA LINDI WAMSHUKURU RAIS SAMIA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA

Written by mzalendoeditor

Siku mbili baada ya kuzindua kampeni ya msaada wa kisheria wa Mama Samia Mkoani Lindi wananchi wa halmashauri ya Manispaa ya Lindi wamemshukuru Rais Samia suluhu Hassan kwa kuwapelekea huduma hiyo ambayo imekuwa msaada Katika ufumbuzi wa matatizo Yao ya kisheria

Wakizungumza wakati wa kupata huduma hiyo wananchi wa mitaa ya Mtele, Mmakonde na Sokoni Kata ya Mingoyo wamesema kampeni hiyo imekuwa msaada kwao Katika kupata ufumbuzi wa matatizo Yao

Mratibu wa kampeni hiyo Katika Manispaa ya Lindi Hosana mgeni Amesema kampeni hiyo ya msaada wa kisheria kwa Manispaa hiyo itafikiwa Katika kumi ikihusisha mitaa 10 kwa kila Kata hizo

Katika kampeni hiyo licha ya kutatua na kusikiliza matatizo ya wananchi pia maafisa hao wametoa Elimu mbalimbali juu ya maswala ya Aridhi, ndoa, mirathi na ukatili wa kijinsia hapa mwanasheria wa Halmashauri Manispaa hiyo erasto ng’ombo anaeleza Umuhimu wa kuacha wosia

About the author

mzalendoeditor