Na Gideon Gregory, Dodoma.
Malalamiko dhidi Mkuu wa Chuo cha Taasisi ya Uhasibu Arusha (IAA), Prof. Eliamin Sedoyeka yameendelea kusikilizwa leo mbele ya Baraza la Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma kwa makosa Manne ya kukiuka maadili ya viongozi wa umma.
Kitika kikao hicho cha kusikiliza tuhuma dhidi ya Mkuu huyo ambacho kimefanyika katika ukumbi wa makao makuu ya ofisi ya Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma Jijini Dodoma chini ya mwenye kiti Mhe.Jaji ( Mst) Rose Teemba na wajumbe wa Baraza hilo Bw.Peter Ilomo na Suzan Mlawi.
Katika kikao hicho upande wa mlalamikaji ulileta wengine na kufikia Sita ambapo miongoni mwao yupo Ramadhan Juma ambaye ni Afisa uchunguzi wa sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma Makao makuu Dodoma pamoja na baadhi ya watumishi wa chuo cha IAA na upande wa mlalamikiwa haukuwa na mashahidi.
Akijitetea mbele ya Baraza hilo Prof. Sedoyeka ameyakana baadhi ya mashitaka na kuliomba baraza limfutie mashitaka yote kwa madai ya kuwa alifanya hivyo kwa lengo la kukuza maendeleo ya chuo hicho na Taifa kiujumla.
“Mhe.mwenyekiti katika suala la kumpandisha cheo Bw.Hakimu Ndatama hapa kiukweli sikumpandisha cheo maana sikuwa na mamlaka ya kumpandisha cheo kilicho fanyika ni uteuzi wa kumpangia majukumu, wakati mwaka jana narudishwa IAA katika Idara kulikuwa na mtumishi mmoja kilichokuwa kinafanyika ni kwamba kazi zote silizokuwa zinahusiana na Raslimali watu zilikuwa pamoja ikawa inapelekea idara kutokufanya vizuri maana upande mmoja ulikuwa unapewa kipaumbele mwingine haupewi.
“Katika suala la uhusiano wa karibu na Bw. Hakimu Mhe.Mwenyekiti wakati mimi narudi kuwa mkuu wa chuo cha IAA na Bw. Hakimu aliniambia na yeye alikuwa anamchakato wa kurudi IAA kwahiyo mimi sikuhusika kumrudisha niliambie baraza lako sina hatia katika shitaka hili,”amesema.
Baada ya kusikiliza pande zote mbili Mwenyekiti wa Baraza alimueleza mlalamikiwa kuwa wamepokea ushahidi kutoka pande zote mbili kilicho baki ni baraza kuwasilisha shauri sehemu husika.