Featured Kitaifa

TASAC WATOA ELIMU YA USALAMA KWA WAVUVI WILAYANI MKINGA

Written by mzalendoeditor
Ofisa Mfawidhi wa Shirika hilo Mkoani Tanga
Captain Christopher Shalua kulia akitoa elimu kwa wavuvi, wamiliki wa vyombo
wa Vijiji vya Petukiza na Moa wilayani Mkinga kuhusu usalama na umuhimu wa kuwa na vifaa vya kujiokolea ikiwemo maboya
wakati wanapokuwa wakifanya shughuli zao za majini kila siku.
Ofisa Mfawidhi wa Shirika hilo Mkoani Tanga
Captain Christopher Shalua kulia akitoa elimu kwa wavuvi, wamiliki wa vyombo
wa Vijiji vya Petukiza na Moa wilayani Mkinga kuhusu usalama na umuhimu wa kuwa na vifaa vya kujiokolea ikiwemo maboya
wakati wanapokuwa wakifanya shughuli zao za majini kila siku.

Ofisa Mfawidhi wa Shirika hilo Mkoani Tanga
Captain Christopher Shalua akiwaonyesha wavuvi kifaa cha kuzimia moto ambacho ni muhimu viwepo kwenye vyombo vyao

Mwenyekiti wa
Kitongoji cha Kijiji cha Petukiza Kata Moa wilayani Mkinga Mrashi Kea
Kasim akizungumza kushoto ni Ofisa Mfawidhi wa Shriika la Tasac Mkoani Tanga Captain Christopher Shalua
AFISA Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la TASAC Kitengo cha Mahusiano na Masoko Amina  Miruko akieleza jambo wakati wa utoaji wa elimu hiyo
OFISA Mfawidhi wa TASAC Mkoa wa Tanga Captain Christopher Shalua kushoto akiwaonyesha wavuvi namna ya kuweza kuvaa moja ya  vifaa vya kujikolea wanapokuwa wakiingia majini kufanya shughuli zao za kila siku
OFISA Mfawidhi wa TASAC Mkoa wa Tanga Captain Christopher Shalua kushoto akisisitiza jambo kulia ni AFISA Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la TASAC Kitengo cha Mahusiano na Masoko Amina  Miruko

NA OSCAR ASSENGA, MKINGA.

SHIRIKA la Uwakala wa Meli
Tanzania (TASAC) Mkoa wa Tanga limekutana na wavuvi, wamiliki wa vyombo
wa Vijiji vya Petukiza na Moa wilayani Mkinga kwa ajili ya kutoa elimu
ya usalama wa vyombo vya majini na umuhimu wa kuwa na vifaa vya kujiokolea ikiwemo maboya
wakati wanapokuwa wakifanya shughuli zao za majini kila siku.

Akizungumza
wakati akitoa elimu hiyo,Ofisa Mfawidhi wa Shirika hilo Mkoani Tanga
Captain Christopher Shalua alisema vyombo vidogo vya majini vinapaswa
kuzingatia usalama na utunzaji wa mazingira ikiwemo matumizi sahihi ya
maboya ya kujiokolea.

Alisema pia ni muhimu wakatambua matumizi
sahihi wakati wa kuyavaa kutokana na muhimu kuyavaa muda wote wanapokuwa
kwenye shughuli za uvuvi au kusafiri majini ili kuweza kuwasaidia pindi
wanapokumbana na majanga mbalimbali.

Captain Shalua alisema
walikuwa wakiwaelimisha wavuvi ili waweze kupata uelewa juu ya matumizi
sahihi ya vifaa ambavyo kwa mujibu wa sheria vinapaswa kuwepo kwenye
vyombo.

“Lakini pia vifaa vyengine ambavyo vinapaswa kuwepo
kwenye vyombo vyenu ni vya kuzimia moto na vile kwa ajili ya huduma ya
kwanza kwani vina umuhimu wakati wa dharura ni wakati gani mvuvi anaweza
kuvitumia ili viwe msaada kwake”Alisema Captain Shalua.

Hata
hivyo alisema kwa mfano vyombo vingi vya uvuvi vinatumia mafuta ya
petrol kwa ajili ya kuendesha mashine zao kwa hiyo moto unapowaka
kutokana na mafuta hayo hawawezi kuzima kwa kutumia maji badala yake
wanaweza kuuzima kwa kutumia mchanga au poda maalumu iliyopo kwenye
mitungi.

Aliongeza kwamba pia wanaweza kutumia mapovu maalumu
yaliyopo kwenye mitungi hivyo elimu yao ilijikita kwenye maeneo hayo ili
iweze kuwasaidia wavuvi wanapokuwa mbali na nchi kazi wanapopata
majanga ya waweze kujisaidia na kuokoa mali na kuwaepusha na kupoteza
maisha.

Awali akizungumza wakati wa mkutano huo Mwenyekiti wa
Kitongoji cha Kijiji cha Petukiza Kata Moa wilayani Mkinga Mrashi Kea
Kasim alisema wavuvi wamesikiliza elimu hiyo na changamoto kubwa wavuvi
wamekuwa wamekufa baharini kutokana na kuwa na vifaa vya kujiokolea.

“Tunaiomba
Serikali ione namna ya kutusaidia wavuvi nasi baadae tuweze kununua
kwani ni ukweli kwamba wavuvi wanapotoka nchi kavu kwenda baharini kuna
urefu mkubwa na mtu anaachwa mita 20 pekee yake bila msaada na wakati
mwengine kujiokoa anapopata dhoruba inakuwa ni mgumu”Alisema

Alisema
kutokana na kwamba Serikali inaingiza mapato makubwa sana kutokana na
ukusanyaji wa maduhuli hivyo wanaiomba iwaangalie kwa unyonge kwa
kuwawezesha ili baadae waweze kujinunulia wenyewe vifaa vya usalama.

Naye
kwa upande wake Mkazi wa Kijiji cha Petukiza Kasim Ally alisema kwamba
elimu hiyo itakwenda kuwasaidia wakati wakitekeleza shughuli zao
mbalimbali za uvuvi .

“Kwanza nilishukuru shirika la Tasac kwa
kuona umuhimu wa kuja kutupa sisi wavuvi elimu na tunahaidi tutakwenda
kuifanyia kazi kwa mapana makubwa “Alisema Kasim.

About the author

mzalendoeditor