HALI ya Chelsea imezidi kuwa mbaya katika Michuano mbalimbali baada ya jana kupoteza jumla ya mabao 3-1 dhidi ya Real Madrid kwenye mchezo wa kwanza wa Robo Fainali usiku huu Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
Shujaa wa Real Madrid alikuwa mshambuliaji Mfaransa, Karim Benzema aliyefunga mabao yote matatu dakika ya 21, 24 na 46, wakati la Chelsea limefungwa na Kai Havertz dakika ya 40.
Kwa ushindi huo Real Madrid wametanguliza mguu moja Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya wenyeji, Chelsea