Featured Kitaifa

ELIMU YA FEDHA YAWAFIKIA WANANCHI WA MKURANGA

Written by mzalendo

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Bw. Waziri Kachi Kombo, akipitia vipeperushi vyenye taarifa za elimu ya fedha alivyokabidhiwa na Afisa Usimamizi wa Fedha Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Grace Muiyanza, ofisini kwa Mkurugenzi, wakati Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Fedha ilipowasili kwa ajili ya programu ya elimu ya fedha kwa wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga, Pwani.

 Na. Saidina Msangi, Mkuranga Pwani.

Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha, imewasili katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani kwa ajili ya kutoa elimu ya fedha kwa wananchi itakayo wawezesha kuepukana na mikopo umiza pamoja na kujifunza kuhusu, usimamizi wa fedha binafsi, bima, mikopo, dhamana na uwekezaji.

Hiyo itakuwa awamu ya mwisho ya mfululizo wa programu ya elimu ya fedha kwa umma inayotekelezwa na Wizara ya Fedha ambapo mikoa 13 imefikiwa na kupatiwa elimu hiyo hadi sasa huku Mikoa mingine ikitarajiwa kufikiwa hapo baadae.

Timu hiyo imekutana na wananchi na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga na kuwapatia elimu ya fedha ambapo walitoa rai kwa Wizara kuona namna ya kutoa elimu hiyo kwa viongozi ili wawe na uelewa wa pamoja katika kuhudumia wananchi.

Aidha, Timu ilitoa elimu kwa wananchi wa Kijiji cha Mlamleni Kata ya Tambani, Mkuranga na Vikindu ambapo wananchi hao kwa pamoja waliipongeza Wizara kwa jitihada ya kuwafikishia elimu ya fedha na kuomba elimu hiyo itolewe mara kwa mara ili kuweza kuwafikia wananchi wengi zaidi ili kuwa na uchumi jumuishi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Bw. Waziri Kachi Kombo, akipitia vipeperushi vyenye taarifa za elimu ya fedha alivyokabidhiwa na Afisa Usimamizi wa Fedha Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Grace Muiyanza, ofisini kwa Mkurugenzi, wakati Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Fedha ilipowasili kwa ajili ya programu ya elimu ya fedha kwa wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga, Pwani.

Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Bw. Omary Saidi Mwanga, akipokea maelezo kuhusiana na vipeperushi alivyokabidhiwa na Afisa Usimamizi wa Fedha Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Grace Muiyanza, wakati Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Fedha ilipowasili kwa ajili ya programu ya elimu ya fedha kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Pwani.

Afisa Sheria Mwandamizi Kurugenzi ya Ustawi na Huduma Jumuishi za Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Ramadhani Myonga, akitoa elimu ya fedha kwa wakuu wa idara na vitengo wa Wilaya ya Mkuranga, wakati timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Fedha ilipowasili kwa ajili ya programu ya elimu ya fedha kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Pwani.

Mchumi Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Gibson Sabayo, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mlamleni Kata ya Tambani, Mkuranga, kuhusu elimu ya fedha wakati Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Fedha ilipowasili kwa ajili ya programu ya elimu ya ya fedha kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Pwani.

 

Wananchi wakichangia mada katika majadiliano baada ya mafunzo ya elimu ya fedha kutolewa na Maafisa kutoka Wizara ya Fedha, walipowasili kwa ajili ya programu ya elimu ya fedha kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Pwani.

Baadhi ya wananchi wa Vikindu  katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa na Maafisa kutoka Wizara ya Fedha waliowasili kwa ajili ya programu ya elimu ya fedha kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Pwani.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Mkuranga -Pwani)

About the author

mzalendo